Tuesday 18 September 2012

DIWANI ENDIAMTU

Diwani wa kata ya Endiamtu Lucas Zacharia akizungumza kwenye kikao cha mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara

1 comment:

  1. MWENYEKITI wa mtaa wa Sekondari Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,Hussein Msokoto amechaguliwa tena kuwa Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji huo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

    Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo ulifanyika juzi,Ofisa Tarafa ya Moipo,Joseph Mtataiko alisema Msokoto (CCM) alipata kura 11 na Said Kuzecha (Chadema) alipata kura moja kati ya kura 12 zilizopigwa.

    Mtataiko alisema Diwani wa Kata ya Endiamtu Lucas Zacharia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira na Joseph Masasi amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,Afya na Maji.

    Kwa upande wake,Ofisa Mtendaji wa mji huo,Nelson Msangi aliwataja wajumbe wa Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ni Albert Siloli,Hussein Msokoto,Lucas Zacharia,Joseph Masasi,Aurelia Michael na Prim Barnabas.

    Msangi alisema kuwa Hussein Msokoto anakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti Ukimwi kupitia nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti na wajumbe ni Albert Siloli,Wilbert Nyari na Aurelia Michael.

    “Uchaguzi huu umetokana na waraka unaotutaka Mamlaka ya miji kufanya uchaguzi kila mwaka kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti pamoja na kamati zote nne za kudumu za mamlaka yetu,” alisema Msangi.

    Akifunga mkutano huo wa uchaguzi,Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo,Albert Siloli aliwapongeza wajumbe wote waliochaguliwa kwenye kamati hizo na aliwataka kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa jamii.

    Msangi aliwataka wajumbe hao kutoa ushirikiano kwa watumishi wa Mamlaka hiyo ili kuhakikisha mji huo unakusanya mapato ya kutosha yakuweza kufanya Mirerani ipatiwe hadhi ya mji kamili.

    “Tuwape watumishi wa Mamlaka yetu ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha ya kwamba mapato yanaongezeka katika vyanzo mbalimbali ili tuweze kunufaisha mji wetu ambao kwa hivi sasa unazidi kukua kwa kasi,” alisema Siloli.

    MWISHO.

    ReplyDelete