Saturday, 15 September 2012

AZIMIO LA ARUSHA

Azimio la Arusha

1 comment:

 1. WAJUMBE wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamesusia kuhudhuria vikao vya Baraza la Mamlaka hiyo kushinikiza walipwe madeni ya posho za vikao hadi kufanikiwa Halmashauri hiyo kuwarudishia vyanzo vyao vya mapato.

  Hayo yameelezwa jana na Mjumbe wa Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango Editha Momo wakati akisoma azimio la wajumbe wa Kamati hiyo kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani.

  Momo alisema wajumbe wa Mamlaka hiyo waliazimia kugoma kuhudhuria vikao vya Baraza hilo kwani tangu Agosti mwaka 2008 Mamlaka hiyo ilipoanzishwa hawakulipwa posho za vikao hadi hivi sasa hivyo kuwakwamisha.

  “Tunashangazwa na kitendo cha kutopewa kipaumbele kwa kulipwa posho zetu kwani wabunge huwa wanapewa fedha za posho za vikao lakini sisi tumekuwa tunajitolea bila kulipwa kwa muda wote huo,” alisema Momo.

  Hata hivyo,Ofisa Mtendaji wa mamlaka hiyo,Nelson Msangi alithibitisha wajumbe wa mamlaka hiyo kudai sh12.5 milioni za posho za vikao hadi wakagoma na shughuli kufanywa na kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango.

  Msangi alisema posho za vikao hazitaleta usumbufu tena kwani Halmashauri hiyo imewaachia vyanzo vya mapato vya sh1.750 milioni kila mwezi ambavyo ni soko na mnada wa Songambele,machinjio na kituo cha magari ya abiria.

  Pia,wajumbe wa mamlaka hiyo waliridhia wazo la Diwani wa Kata ya Mirerani Justin Nyari la kumtaka Mkurugenzi wa halmashauir hiyo Alhaji Muhammad Nkya kumpunguzia majukumu Msangi ambaye bado ni Ofisa Ushirika wa wilaya hiyo.

  Naye,Diwani wa kata ya Endiamtu Lucas Zacharia alisema ushirikishwaji wa viongozi wa Mamlaka hiyo unapaswa kuongezwa ili kuhakikisha kuwa majukumu ya kila mmoja yanatimizwa ipasavyo kwa manufaa ya jamii.

  MWISHO.

  ReplyDelete