Kwanza kabisa
namshukuru Mungu kwa kunijalia kuwa mbunge kwani nilikuwa na maono ya tangu
siku nyingi kuwa mbunge wa Jimbo hili,pia nakishukuru chama changu cha CHADEMA
kwa kunipa ridhaa ya kugombea na pia kwa nafasi ya pekee kwa kweli nawashukuru
sana watu wa Arumeru Mashariki ambao hawakujali umri wangu,hawakujali uwezo
wangu kifedha,hawakujali historia ya familia yangu katika siasa,hawakujali kila
mapungufu ambayo nilikuwa nayo,lakini wakaamua kunichagua….Najua walikuja wengi
na fedha nyingi,najua walikuja wengi na majina makubwa,najua walikuja wengi na
kila aina ya mbwembwe,walikuja wengi na bendi nyingi za muziki,walikuja wengi
wakahonga sana,walikuja wengi wakanitukana sana,walikuja wengi wakanisema
sana…Lakini hatimaye sauti ya wengi imekuwa sauti ya Mungu na lile alilolipanga
Mwenyezi Mungu limekwenda kutimilika,tangu mwanzo nilisema tunaanza na Mungu
tunamaliza na Mungu….Walipoambiwa kuwa mimi ni mdogo kiumri wakasema siendi
Bungeni kupeleka mvi au kupeleka miaka na tena wakasema wanahitaji dogo janja
na siyo kubwa jinga…..Walipoambiwa kuwa mimi sijaoa wakasema siendi Bungeni
kusuluhisha ndoa,walipoambiwa sina kitambi wakasema siendi kucheza mieleka
Bungeni na walipoambiwa mimi ni masikini wakasema tunamuhitaji masikini
mwenzetu…Narudia tena kama nilivyosema mwanzo tumeanza na Mungu na tunamaliza
na Mungu….Kamanda Joshua Nassari mara baada ya kutangazwa kuwa Mbunge Mteule
Jimbo la Arumeru Mashariki Aprili 2 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment