Wednesday, 21 September 2016

MWENGE MANYARA

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akimkabidhi zawadi mkimbiza mwenge kitaifa kutoka mkoa humo Lucia Kamafa baada ya mwenge huo kuwasili kijiji cha Gunge Wilayani Simanjiro.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akisoma taarifa ya mkoa huo mara baada ya mwenge wa uhuru kufika mkoani humo, ambapo miradi ya thamani ya zaidi ya sh7.7 bilioni ilitembelewa.
 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa George Mbijima akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.
  Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa George Mbijima akizindua mradi wa maji kwenye Kijiji cha Gunge Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.
  Mkimbiza mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Nahoda akisalimiana na mkurugenzi wa shirika la Mwedo Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, baada ya mwenge kuzindua jengo hilo.
 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Mbijima akisikiliza maelezo ya ofisa ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, Minde Nanagi wakati akizindua soko na ghala lililotumia sh1 bilioni, (kushoto) ni mkuu wa wilaya hiyo Sara Msafiri na (kulia) ni mkimbiza mwenge kutoka mkoa wa Kaskazini Pemba, Nahoda Makame.
  Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini Flatey Massay akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa maji kwenye eneo hilo.
  Ukiwa Wilayani Simanjiro mwenge wa uhuru pia ulizindua mradi wa biogesi kwenye shule ya msingi Emboreet.
 Kilo 40 na misokoto nane ya bangi ilichomwa moto na pombe haramu ya gongo ilimwagwa mara baada ya mbio za mwenge wa uhuru kuwasili wilayani Kiteto. 

No comments:

Post a Comment