Hii ni taarifa kutoka Tarime mkoani Mara ambako watu 12 wamejeruhiwa
wakati wa mashambulizi ya kurushiana risasi kati ya askari wa JWTZ kituo
cha Nyandoto na polisi wa kituo cha stendi.
Kwa mujibu wa magazeti ya Nipashe na Mwanachi leo, hii ishu ilitokea
wakati Wanajeshi hao walipokua wakijaribu kumchukua Mwanajeshi mwenzao
aliyekamwatwa na polisi hao kwa kosa la kuendesha pikipiki bila kuvaa
kofia (Helmet).
Mashambuliazi hayo ya kurushiana risasi na kupigana ngumi na mateke
yalitokea juzi jioni katika kituo hicho cha stendi ambapo Mganga
Mfawidhi Hospitali ya Tarime alithibitisha kupokea majeruhi 12 na kati
yao wawili ni askari wa JWTZ, Polisi saba na raia watatu.
Kamanda wa Polisi wa Tarime na Rorya, ACP Lazaro Mambosasa alisema Mwanajeshi huyo licha ya kukiuka
taratibu za barabarani aliwatolea lugha za matusi polisi hao jambo
lililowalazimu kumkamata kwa nguvu na wanajeshi wenzake kuingilia kati
na kusababisha vurugu.
Alisema Wanajeshi watatu ambao hawakutajwa majina wameshikiliwa na
polisi kwa kuvunja utaratibu wa usalama huku Mkuu wa Wilaya hiyo John
Henjewele akilaani kitendo hicho cha kurushiana risasi za moto hewani na
kusema ni cha utovu wa nidhamu na kilikwamisha shughuli za watu kwa
muda sababu ya kuhofia usalama wao.
Unataka niwe nakusogezea kila stori inayonifikia zikiwemo pichaz,
video’s na stori zenyewe? niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
twitter instagram na facebook cha kufanya ni kujiunga na mimi kwa
kubonyeza
No comments:
Post a Comment