Friday, 29 November 2013
KIKAO ALAT
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mamlaka ya Serikali za mitaa (Alat) Mkoa wa Manyara, Nicodemus Tarmo (katikati) akiongoza kikao cha wajumbe wa mkoa huo kilichofanyika mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro kushoto ni Makamu Mwenyekiti, Mainge Lemalali na Katibu Omary Mkombole.
NACHANGIA ALAT
Mjumbe wa Jumuiya ya Mamlaka ya Serikali za mitaa (Alat) Mkoa wa Manyara, Gasper Sulle kutoka Wilaya ya Hanang’ Gasper Sulle akizungumza kwenye kikao cha wajumbe wa mkoa huo kilichofanyika mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro.
WANACHAMA WATATU MAMEC WAFUKUZWA
Waandishi watatu wa Klabu ya waandishi wa
habari wa Mkoa wa Manyara, Mamec, wamevuliwa uanachama wao kutokana na kukosa
maadili baada ya kufunga kwa kufuli ofisi ya klabu hiyo.
Uamuzi huo mgumu ulichukuliwa mjini
Babati na wanachama wa Mamec baada ya kusomewa na Mwenyekiti wao Benny Mwaipaja
uamuzi wa kamati ya maadili iliyopendekeza wachukuliwa hatua baada ya wao
kugoma kufika.
Wanachama hao waliwafutia uanachama waandishi
hao ambao ni Charles Masayanyika wa kituo cha ITV na Radio One, Hamida Khalid wa
gazeti la Tanzania Daima na na Tabia Daffo wa Radio Uhuru.
Ilidaiwa kuwa, wanachama hao watatu walifunga
ofisi ya Mamec, Novemba mosi mwaka huu wakidai kuwa hawautambui uongozi uliopo
hivyo uamuzi uliotolewa ni kuwafutia uanachama kutokana na kukosa maadili
“Waandishi hawa waliitwa kwenye kamati ya
Maadili, Usuluhishi na Nidhamu lakini wakagoma kufika hivyo kamati hiyo
ikapendekeza wapewe onyo au adhabu ambayo wanachama wanaona inafaa,” alisema Bw
Mwaipaja.
Pia, wanachama hao walikubali kwa ridhaa yao
kujiuzulu kwa Katibu Mtendaji wa Mamec, Zacharia Mtigandi wa Star TV,
aliyeandika barua ya kujiuzulu ambapo nafasi yake itashikiliwa na Abraham
Mlundi wa gazeti la Ohayoda.
Pamoja na hilo wanachama hao waliridhia
kujiuzulu kwa mjumbe wa kamati tendaji, Hamida Khalidi ambapo nafasi yake
ilijazwa na Joseph Simba wa gazeti la Ohayoda.
Makamu Mwenyekiti wa Mamec, Mary Margwe
alisema hatua hiyo ya kuwafukuza uanachama waandishi hao imechukuliwa ili
kuleta nidhamu kwenye chama na watachukua hatua kali endapo hali hiyo
itajitokeza tena.
“Bora tubaki wanachama wawili wenye malengo ya
kutumikia jamii kwa ufasaha kuliko kuwa na kundi kubwa la wanachama, sisi tupo
17 tu lakini tunaanza kufunga ofisi badala ya kuleta hoja mezani,” alisema
Margwe.
Hata hivyo, wanachama wa Mamec, wamepongeza
hatua hiyo ya kufukuzwa uanachama waandishi hao watatu kwani ni muda mrefu
walikuwa wanasababisha fujo zenye lengo la kuanzisha migogoro.
Friday, 15 November 2013
WADAU MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA KATIKA MKOA WA MANYARA
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria kikao cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kilichofanyika Mjini Babati kulia kwake ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya mfuko huo, Lydia Choma na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Babati, Khalid Mandia akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Martha Umbulla na Mkurugenzi wa Uhai na Takwimu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Michael Mhando baada ya kufungua kikao cha wadau wa mfuko huo wa mkoa huo.
Subscribe to:
Posts (Atom)