Waziri Mkuu mstaafu
Fredrick Sumaye akisindikizwa na baadhi ya viongozi wa jadi wa Wilaya ya
Hanang' Mkoani Manyara, kwenda kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
jana mjini Katesh na kuandaliwa na umoja wa Vijana wa CCM wilayani humo.
Baadhi
ya wakazi wa Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu
mstaafu na mbunge mstaafu wa jimbo la Hanang' Fredrick Tluway Sumaye
aliyezungumza nao jana kuhusiana na mambo mbalimbali ya wilaya hiyo na
Taifa kwa ujumla.
Madereva wa
pikipiki wakiwa kwenye maandamano ya pikipiki katika mji mdogo wa Katesh
Wilayani Hanang' Mkoani Manyara, ambapo vijana hao walijipanga kumpokea Waziri
Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye aliyefanya mkutano na kuzungumza na wananchi wa
wilaya hiyo juu ya hali ya kisiasa nchini.
No comments:
Post a Comment