Mratibu wa mradi wa ruzuku kwa
wanaandishi wa habari wa mfuko wa waandishi wa habari nchini (TMF) Danstan Kamanzi
(kushoto) akimkabidhi mjini Dodoma, Mwenyekiti wa kikundi cha waandishi wa
habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) Ramadhan Msangi
moja kati ya kompyuta ndogo (tablet) kwa ajili ya kufanya shughuli za kikundi
hicho.
Mratibu wa mradi wa ruzuku kwa
wanaandishi wa habari wa mfuko wa waandishi wa habari nchini (TMF) Danstan Kamanzi
akizungumza mjini Dodoma na kikundi cha waandishi wa habari 17 wanaoandika habari
za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) kwenye mafunzo ya siku tano ya kuandika
habari za mitandao ya jamii yanayofanyika Dodoma hotel.
Waandishi wa habari 17 wa kikundi
cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) wakiwa
mjini Dodoma kwenye mafunzo ya siku tano ya kujengewa uwezo wa kuandika habari
kwa njia ya mitandoa ya kijamii (social media) yanayoendeshwa na mfuko wa waandishi wa habari nchini TMF.
No comments:
Post a Comment