Tuesday, 31 March 2015

MKUTANO WA SUMAYE KATESH HANANG'



Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akisindikizwa na baadhi ya viongozi wa jadi wa Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara, kwenda kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana mjini Katesh na kuandaliwa na umoja wa Vijana wa CCM wilayani humo.



Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu mstaafu na mbunge mstaafu wa jimbo la Hanang' Fredrick Tluway Sumaye aliyezungumza nao jana kuhusiana na mambo mbalimbali ya wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla.



Madereva wa pikipiki wakiwa kwenye maandamano ya pikipiki katika mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang' Mkoani Manyara, ambapo vijana hao walijipanga kumpokea Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye aliyefanya mkutano na kuzungumza na wananchi wa wilaya hiyo juu ya hali ya kisiasa nchini.

Monday, 23 March 2015

MAFUNZO YA TMF KWA SAUTI YA MNYONGE



Mratibu wa mradi wa ruzuku kwa wanaandishi wa habari wa mfuko wa waandishi wa habari nchini (TMF) Danstan Kamanzi (kushoto) akimkabidhi mjini Dodoma, Mwenyekiti wa kikundi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) Ramadhan Msangi moja kati ya kompyuta ndogo (tablet) kwa ajili ya kufanya shughuli za kikundi hicho.



Mratibu wa mradi wa ruzuku kwa wanaandishi wa habari wa mfuko wa waandishi wa habari nchini (TMF) Danstan Kamanzi akizungumza mjini Dodoma na kikundi cha waandishi wa habari  17 wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) kwenye mafunzo ya siku tano ya kuandika habari za mitandao ya jamii yanayofanyika Dodoma hotel.



Waandishi wa habari 17 wa kikundi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) wakiwa mjini Dodoma kwenye mafunzo ya siku tano ya kujengewa uwezo wa kuandika habari kwa njia ya mitandoa ya kijamii (social media) yanayoendeshwa na mfuko wa waandishi wa habari nchini TMF.

AJALI MIGODINI







Mmiliki wa mmoja kati ya migodi 15 ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Blandina Mkenga akielezea namna moto ulivyozuka na kuunguza mali katika migodi yao.