Wednesday, 2 July 2014

HUDUMA ZA KIBENKI KUANZA KUTOLEWA NA CRDB TAWI LA BABATI MKOANI MANYARA


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo akiwa na wadau mbalimbali wa mkoa huo, wakiwa kwenye Tawi la Babati la Benki ya CRDB ambalo jana lilianza kutoa huduma ya fedha kwa wateja wake, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Khalid Mandia, akifuatiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara, Ndeng'aso Ndekubali na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Omary Chambo na Meneja wa Benk ya CRDB Kanda ya kaskazini Chiku Issa.
Hawa makamanda nao walikuwepo jana wakati Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, lilipoanza kutoa huduma ya fedha kwa wateja mbalimbali mkoani humo ikiwemo kuweka akiba, kutoa fedha na kutoa mikopo.


Meneja wa Benki CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, Ronald Paul akizungumza jana na waandishi wa habari ambapo kwa mara ya kwanza Tawi hilo lilianza kutoa huduma ya fedha kwa wateja wake jana na linatarajia kuzinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda au Rais Jakaya Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo akizungumza wakati Benki ya CRDB Tawi la Babati lilianza kutoa huduma kwa wateja wake, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Khalid Mandia na kushoto ni Mneja wa Benki CRDB Tawi la Babati Ronald Paul ambapo kwa mara ya kwanza Tawi hilo lilianza kutoa huduma ya fedha kwa wateja wake jana na linatarajia kuzinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda au Rais Jakaya Kikwete.

No comments:

Post a Comment