Friday 3 August 2012

WAANDISHI NA RC KILIMANJARO

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa na waandishi wa habari

1 comment:

  1. MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama amesema zoezi la sensa ya watu na makazi litakaloanza Agosti 26 mwaka huu litafainikiwa endapo waandishi wa habari watatumika kuielimisha jamii.

    Gama akizungumza mjini Moshi juzi wakati akifungua mafunzo ya kuandika habari za sensa kwa waandishi wa habari 140 wa mikoa ya kanda ya kaskazini na mashariki alisema waandishi wakitumia kalamu zao ipasavyo sensa hiyo itafanikiwa.

    “Waandishi wa habari watafanikisha zoezi la sensa kwani shughuli zozote za Serikali haziendi vizuri bila waandishi wa habari kujulisha jamii kupitia gazeti redio na runinga,” alisema Gama.

    Aliwaasa waandishi wa habari kutanguliza uzalendo mbele wakati wa kuandika habari za zoezi la sensa ili jamii ipate uelewa kwa kiasi kikubwa na kutambua umuhimu wa sensa ya watu na makazi ambayo mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2002.

    Aliwataka waandishi hao kutanguliza uzalendo wakati wa kuandika habari za sensa kwani jamii ikielezwa habari potofu kupitia waandishi zoezi zima halitafanikiwa ipasavyo kwani wana nguvu kubwa ya kufikisha ujumbe.

    “Hata mimi mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya tukitembelea kwa muda wa miezi mitatu kwenye eneo letu hatutaweza kuwafikia na watu wengi lakini kupitia waandishi wa habari watu wengi watatusikia,” alisema Gama.

    Kwa upande wake,Ofisa uhamasishaji sensa wa Taifa,Said Ameir alisema sensa hiyo itafanyika Agosti 26 na itafanyika kwa muda wa siku saba hivyo jamii inatakiwa itambue kuwa zoezi hilo halitafanyika kwa siku moja.

    Ameir alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni sensa kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa na pia zoezi hilo halitafanyika kwa wananchi kupanga foleni kama wakati wa kura ila makarani wa sensa watatembelea majumbani.

    Alisema ikiwa usiku wa kuamkia siku ya sensa mgeni akilala kwenye kaya na akaondoka kabla ya karani wa sensa hajafika,anatakiwa kuhesabiwa kule alipolala na siyo atakapokutwa baada ya siku ya sensa.

    MWISHO.

    ReplyDelete