Friday, 10 August 2012

LOWASSA NA SENDEKA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Edward Lowassa akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara Christopher Ole Sendeka

1 comment:

 1. WAKAZI wa Mkoa wa Manyara wameupongeza msimamo mkali ulioonyeshwa na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha,Edward Lowassa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama pindi Malawi ilipodai kuwa Ziwa Nyasa lote ni mali yao.


  Wameyasema hayo baada kuripotiwa na vyombo vya habari kuwa Malawi imeondoa ndege zilizokuwa zinazunguka Ziwa Nyasa upande wa Tanzania kufanya utafiti wa mafuta baada ya kauli ya Lowassa kuwa jeshi lipo tayari kwa lolote.


  Walisema baada ya Serikali ya nchi hiyo kusikia kwenye vyombo vya habari vya kimataifa kuwa Lowassa ametangaza kuwa majeshi ya Tanzania yapo tayari kwa vita ili kudai haki yake imewafanya Malawi kuondoka mara moja katika eneo hilo.


  Mkazi wa mji mdogo wa Mirerani Ghulam Obela alisema Tanzania inahitaji kuwa na viongozi wenye kuweza kutoa uamuzi mgumu wa mara moja kama Lowassa ambao wanauelewa mpana kuwa haki haiombwi ila inadaiwa.


  “Mara baada ya Lowassa kutamka hivyo Serikali ya Malawi ikatambua kuwa hatari inakuja mbele yao wakabaini kwamba suluhu ni kuondoka mara moja kwenye eneo hilo bila hivyo tungewasambaratisha vibaya,” alisema Obela.


  Alisema Lowassa amefuata nyayo za Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1963 na 1970 aliyekuwa Rais wa Malawi Kamuzu Banda aliingiza majeshi yake eneo hilo na Nyerere akamwambia aondoke kabla hajampiga na Banda akatii amri hiyo.


  Mkazi wa Simanjiro George Martin alisema maamuzi magumu ya Lowassa yamesababisha Malawi kuondoka kwa kuogopa kupigwa kwani hakumumunya maneno mdomoni wala hakunong’ona ila alizungumza waziwazi bila uoga.


  “Lowassa ni miongoni mwa viongozi wenye kuonyesha udhubutu kwani baada ya kutamka kuwa Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani kama itabidi ndege za Malawi zikaondoka Ziwa Nyasa mara moja,” alisema Martin.


  Juma Hamis wa mjini Babati alisema viongozi wengine wanatakiwa kuiga mfano wa Lowassa kwani kiongozi anapaswa kuzungumzia jambo moja kwa moja kuliko kuingiza siasa na maneno yasiyo na msingi au kubembelezana.


  “Lowassa ni miongoni mwa viongozi walioacha alama hapa nchini na atazidi kukumbukwa kwani ubunifu wa shule za kata maarufu kama sekondari za Lowassa na pikipiki za bodaboda zimetoa ajira kwa vijana,” alisema Hamis.


  Alisema kauli ya Lowassa imetoa picha kwa nchi ya Malawi kuonyesha na kutambua aina ya viongozi wa Tanzania ilionao ambao wana msimamo mkali usiorudi nyuma katika kudai haki yao ya msingi.


  MWISHO.

  ReplyDelete