Monday 13 August 2012

FATHE GASTO NA ZAWADI YA GARI

Father Gasto Sinkala akikabidhiwa gari lake aina ya Suzuki Escudo alilopewa na wakazi wa mji mdogo wa Mirerani Wilaya y a Simanjiro Mkoani Manyara

1 comment:

  1. WAAMINI wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozali wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara wamempa zawadi ya gari padri Gasto Sinkala ambaye amepata upadri hivi karibuni mjini Arusha.

    Akizungumza wakati wa misa ya shukrani ya kupata upadri iliyofanyika kwenye Parokia ya Mirerani,Mwenyekiti wa kamati ya misa hiyo,Nobert Olomi alisema gari hilo aina ya Suzuki Escudo lina thamani ya sh11 milioni.

    Olomi alisema waamini wameona wampe zawadi ya gari hilo ili kumrahisishia usafiri padri Sinkala kwenye eneo lake la uinjilishaji huko Loliondo na pia awakumbuke waamini wa Mirerani kwa sala kila akilitumia gari hilo.

    Akitoa shukrani kwa waamini wa kanisa hilo wakiongozwa na mapadri wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha,Pastory Kijuu,Aloyce Kitomari,Raphael Loratare na Theopil Mroso,Padri Sinkala alisema anamshukuru Mungu kwa kufanikisha wito wake.

    Padri Sinkala alisema japokuwa amelelewa katika mazingira na mikono ya watu tofauti wakiwemo wazazi na ndugu zake hatimaye amefanikiwa kupata daraja la upadri ambalo alikuwa na wito nao tangu akiwa mdogo.

    “Namshukuru Mungu hata kunifikisha hapa leo ingawa wazazi wangu wapo hai lakini hivi sasa wapo nyumbani Mbeya hawajashuhudia umati huu uliopo leo hii lakini furaha yangu na yenu ndiyo furaha yao pia,” alisema Padri Sinkala.

    Kwa upande wake,Padri Mroso ambaye ni mlezi wa imani wa Padri Sinkala alisema waamini wa Mirerani wameweka rekodi kwa kununulia gari ambalo litamsaidia Padri huyo kwenye uinjilishaji.

    “Mirerani mpo juu kwani katika historia ya Jimbo Katoliki la Arusha hakuna padri aliyepewa gari na waamini ninyi ni wa kwanza nadhani vijana wa Mirerani miaka ijayo wakipata upadri mtawapa helkopta au ndege,” alisema Padri Mroso

    Naye,Padri Pastory Kijuu aliyekuwa Paroko wa Kanisa Katoliki Mirerani na ambaye anasoma chuo kikuu cha Nairobi alisema kila shughuli za kichungaji atakayofanya Padri Sinkala watu wa Mirerani watabarikiwa.

    Paroko mpya wa Kanisa Katoliki Mirerani,AlouKitomari alifurahishwa na kitendo cha waamini hao kumpa gari Padri Sinkala kupewa gari ambalo litamsaidia kufanya uinjilishaji huko Loliondo,Dikodiko na Samunge wilayani Ngorongoro.

    “Mimi nilipoanza upadri mwaka 1981 nilikuwa natumia baiskeli hivyo nawapongeza kwa kumtunza gari Padri Sinkala japokuwa hata asingepata hilo gari angetoa huduma ya upadri bila matatizo,” alisema Padri Kitomari.

    MWISHO.

    ReplyDelete