Sunday, 29 July 2012

DOGO MAONI YA KATIBA


Mwanafunzi wa shule ya msingi Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara akitoa maoni yake kwenye katiba mpya

CHETI CHA ULINZI SHIRIKISHI


MAONI YA KATIBA

KIKIARAkdia
Add caption

RC AKIKAGUA GWARIDE

Mkuuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwilo akiongozana na Kamanda wa polisi wa mkoa huo ili kukagua gwaride la askari polisi wakati akigawa vyeti na fedha kwa askari wa jeshi hilo waliofanya vitendo vya kuigwa mfano

Tuesday, 17 July 2012

MABINGWA BONANZA

Mbunge wa Vitimaalum Vijama mkoani Arusha (CCM) Catherine Magige akimkabidhi kombe mchezaji wa timu ya Arusha Journalis Training College baada ya kushinda mashindano ya Bonanza Arusha kulia ni Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela.

BONAZA TASWA ARUSHA

Mgeni rasmi wa bonanza la waandishi wa habari wa lililoandaliwa na waandishi wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Arusha kupitia Kampuni ya MS Unique ya mjini Arusha,Mbunge wa Viti maalum CCM Vijana Mkoa wa Arusha,Catherin Magige akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongella kulia ni Mratibu wa Bonanza hilo Jamillah Omary na wapili kulia ni mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo.

Friday, 13 July 2012

MKOMANZI

Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro

Thursday, 12 July 2012

NAIBU WAZIRI


Joseph Lyimo,Mirerani
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini,Stephen Masele ameiamuru kampuni ya TanzaniteOne kuacha kumwaga maji kwenye migodi ya wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Akizungumza na uongozi wa kampuni hiyo,Masele ambaye ni Naibu Waziri anayeshughulikia madini aligeuka na kuwa mkali mithili ya mbogo wakati akizungumzia suala hilo kwa viongozi wa kampuni hiyo.

Naibu waziri alitoa amri hiyo baada ya kuelezwa na wachimbaji wadogo alipofanya ziara ya kutembelea migodi yao kuwa kampuni hiyo inawamwagia maji mgodini na alipotoa amri hiyo gari lake lilisukumwa na wachimbaji hao.

“Sawa hawa ni wawekezaji lakini Serikali haipo tayari kuona wachimbaji wadogo wananyanyaswa katika nchi yao hivyo nimeiamuru kampuni hiyo kusitisha mara moja kumwaga maji hayo,” alisema Masele.

Hata hivyo,Mwenyekiti wa kampuni ya TanzaniteOne,Ammi Mpungwe alimthibitishia Masele kuwa kampuni yake haimwagi maji kwenye migodi ya wachimbaji wadogo ila maji hayo yanatoka yenyewe kwenye mgodi wa TanzaniteOne. 

Mpungwe alisema maji hayo hutoka nyenyewe kutokana na jiolojia ya miamba ilivyo kwenye mgodi wao wa Bravo ambao haufanyiwi kazi lakini kampuni hiyo haijawahi kumwaga maji kwenye migodi ya wachimbaji wadogo.

“Mheshimiwa waziri mimi nilikuwa balozi na nikastaafu kwa heshima zote,sasa siwezi kwenda jela leo kwa kosa la kukiuka sheria za nchi,mimi ni mzalendo sitakubali kuruhusu kampuni yetu imwage maji migodini,” alisema Mpungwe.

Pia,Naibu Waziri huyo aliitaka kampuni hiyo kusaidia huduma za jamii kama madawati shuleni,afya na maji kwenye kata zote nne za tarafa ya Moipo wilayani humo kuliko kuisaidia kata moja ya Naisinyai.

“Watanzania hawatatuelewa ikiwa kampuni hii inachimba madini ya Tanzanite yenye utajiri mkubwa wakati kata za jirani wanafunzi wanakaa  sakafuni,huduma za afya duni na barabara ya Kia-Mirerani ni ya vumbi,” alisema Masele.

Akizungumzia kuhusu hilo,Mpungwe alisema watajipanga kulitekeleza ila alisikitishwa na kitendo cha viongozi wa kilichokuwa kijiji cha Mirerani kukataa msaada wa zaidi ya sh12 milioni walizotoa kama msaada wa maendeleo mwaka 2000.

MWISHO.

Monday, 9 July 2012

WAANDISHI WAKIWA MJINI MOSHI KWENYE SEMINA YA TANAPA


Add caption
Add caption

HALMASHAURI MANYARA

Add caption

TANAPA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Taifa TANAPA Allan Kijazi akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa ya Manyara,Kilimanjaro,Tanga,Arusha na Dar es salaaam kwenye semina ya TANAPA inayofanyika mjini Moshi