Monday, 25 June 2012

MAKAMANDA KASKAZINI

Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Liberatus Sabas kushoto akizungumza na Makamanda wa mikoa ya Manyara,Akili Mpwapwa kushoto na Robert Boaz wa Kilimanjaro kwenye kikao cha ujirani mwema wa viongozi wa Kanda ya Kaskazini kilichofanyika mjini Babati

DC NA MATREKTA

Mkuu wa wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara,Christint Mndeme akiwasha trekta moja kati ya matrekta tisa yaliyotolewa kwa mkopo kwa kikundi cha Takauma SACCOS cha Tarafa ya Bassotu mkopo huo uliwezeshwa na Mbunge wa Viti maalum Mkoani Manyara Chadema,Rose Kamil Sukums.

Saturday, 23 June 2012

MADAWATI HATUNA

Mwanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay Mjini Babati akizungumza kwenye mdahalo wa uwajibikaji wa viongozi uliondaliwa na Mtandao wa asasi za kijamii mkoani Manyara MACSNET na kufadhiliwa na The Foundation For Civil Society.

UJIRANI MWEMA

Mkuu wa Mkoa Manyara Elaston Mbwilo,Elaston Mbwilo akifungua mkutano wa ujirani mwema baina ya mikoa ya Manyara,Arusha,Kilimanjaro na Manayara uliofanyika Juni 23 Mjini Babati

Tuesday, 19 June 2012

JK

Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Kamishna Salma Abdi Chande wa Tume ya Usuluhishi na Upatanishi

MNYIKA

Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mheshimiwa John Mnyika akiwa na askari wa Bunge baada ya kutolewa ndani ya Bunge leo na Naibu Spika wa Bunge Mh Job Ndugai alipotamka Bungeni kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu

JK

Rais Jakaya Kikwete na baadhi ya waandishi wa habari mjini Arusha

Sunday, 17 June 2012

USHIRIKINA KWA MTOTO WAKO

Mtoto Monica Anthony (3) akihojiwa na askari polisi wa upelelezi Neema Lucas na Sajini Joseph Mirambo wa kituo cha polisi Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambaye amekuwa akifanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo kujeruhiwa kwa vipigo na kufanyiwa ushirikina na baba yake mzazi Anthony Bedan (25) ambaye amekuwa akimlaza kwenye uvungu wa kitanda na kumpiga ili kumtoa damu ili ajipake akapate madini ya Tanzanite mgodini ambapo pia humning'iza mtoto wake Christina Anthony (9) wapili kushoto miguu juu kichwa chini ili damu zimtoke puani kisha amwagie Monica ili akapate madini kwa vitendo vya ushirikina. 

Thursday, 14 June 2012

PUNDAMILIA

Punda milia wa hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro

TWIGA WA NGORONGORO

Twiga wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Margareth Zziwa akizungumza mjini Arusha baada ya kuchaguliwa hivi karibuni

MAGUFULI

Jengo la Lusona House likiwa limevunjwa na wamiliki wake kwa amiri ya waziri wa Ujenzi John Magufuli