Monday 28 November 2016

MAHAFALI YA PILI SHULE YA SEKONDARI MGUTWA SIMANJIRO


Meneja wa shule ya sekondari Mgutwa ya Kijiji cha Kandasikira, Wilaya ya  Simanjiro Mkoani Manyara, Monica Mlemeta akizungumza kwenye mahafali, (wa pili kushoto) ni mgeni rasmi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, Kazimbaya Makwega na Mkurugenzi wa taasisi ya Agape Mission International inayomiliki shule hiyo Canon Kedmon Mlemeta.


Wanafunzi 65 wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Mgutwa inayomilikiwa na taasisi ya Agape Mission International, iliyopo Kijiji cha Kandasikira Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye mahafali ya pili ya shule hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, Kazimbaya Makwega, akimpa zawadi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mgutwa iliyopo Kijiji cha Kandasikira, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Isack Chacha, kwenye mahafali ya shule hiyo, kushoto ni meneja wa shule hiyo Monica Mlemeta na wapili kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Agape Mission inayomiliki shule hiyo Canon Kedmon Mlemeta.

No comments:

Post a Comment