Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akizungumza na
wafanyakazi wa shirika la nyumba nchini (NHC) wa jijini Arusha alipofanya ziara
yake.
Monday, 15 February 2016
MANYARA
Diwani
wa Kata ya Terrat Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Ole Materi
akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Wadau
wa madini ya Tanzanzite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara, wakiwa kwenye mkutano wa kamati ya ulinzi na usalama ya kanda ya
kaskazini.
Thursday, 4 February 2016
WATAKA KAMPUNI YA TANZANITEONE IONDOLEWE
Wachimbaji wa kampuni
ya TanzaniteOne ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,
wameiomba Serikali iiondoe kampuni hiyo kwani imeshindwa kujiendesha hadi
kushindwa kuwapa chakula na maji.
Wakizungumza juzi
mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya mikoa ya kanda ya kaskazini, wachimbaji
hao walidai kuwa hivi sasa wanafanya kazi kwenye mazingira magumu kutokana na
uwezo mdogo wa kampuni hiyo kujiendesha.
Mmoja kati ya
wafanyakazi hao Sophia Mbimbi alisema wamekuwa na wakati mgumu wa kufanya kazi
kwani kila siku wanakula chakula cha aina moja na hata maji ya kunywa inabidi
mfanyakazi ajinunulie dukani ili ashuke nayo mgodini.
“Kampuni inayochimba
mgodi mkubwa wa Tanzanite kuliko yote duniani inashindwa kuwa na hata maji safi
na salama na kununua maji yanayotoka wilayani Hai, huko ni kutusononesha na
kutushangaza sana,” alisema Mbimbi.
Mchimbaji mwingine
Aven Mwaitalako alisema kampuni hiyo imeshindwa kufanya kazi kwani tangu wanunue
hisa imekuwa inaendesha mambo yake bila kuwa makini hadi kufikia hatua ya
kupiga nguzo badala ya kubuni eneo.
“Imefikia hatua ya
kufuata nguzo zilizoachwa na mzungu zilizokuwa zinatoa madini na ndizo tunapiga
baruti, badala ya kutafuta njia zetu nyingine ili tuoe madini, kweli kampuni
hii imejichokea,” alisema Mwaitalako.
Kwa upande wake,
Raphael Ombade alisema suala la wafanyakazi kupekuliwa kwa kuvuliwa nguo siyo
zuri kwani ni udhalilishaji wa utu wa
mtu na pia mionzi iliiyokuwa inawapekua awali ilikuwa ya mizigo hivyo
isirudishwe tena.
Hata hivyo, meneja wa
mgodi huo, Modest Apolinary alisema uongozi wa kampuni hiyo umejipanga
kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza na kila wakati watakuwa wanakutana na
uongozi wa wachimbaji ili kujadili kwa pamoja.
“Pamoja na hayo sisi
ni watanzania jamani kwani mlitaka kula chakula gani na haya maji mtaalamu wetu
ametuhakikishia ni masafi na salama kwani yametoka hapo Boma Ngombe wilayani
Hai, hayana tatizo,” alisema.
Akizungumza na
uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni
mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amosi Makala alisema ameiagiza TanzaniteOne
iwekeze fedha nyingi zaidi ili ipate madini zaidi.
“Mtakuwa mnafanya
ubabaishaji sasa, hadi mnapiga nguzo za zamani jamani, wekezeni mtaji mkubwa
ili mpate madini na siyo kuwa kama mnavuna majani na kuokota karanga
zilizobakia shambani,” alisema Makala.
Subscribe to:
Posts (Atom)