Diwani wa Kata ya Bonga, Mjini Babati Mkoani Manyara, Pasian Siay
akizindua mradi wa maji ya kisima kwenye kata yake.
Monday, 26 August 2013
Monday, 19 August 2013
Tuesday, 13 August 2013
MAZISHI YA MAREHEMU ERASTO MSUYA BILIONEA WA MADINI YA TANZANITE
Mkuu wa mkoa wa
Arusha Magesa Malongo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa wa Arusha amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa
inawashikilia wote waliohusika na mauaji ya bilionea mfanyabiashara maarufu wa
madini ya Tanzanite Erasto Msuya.
Akizungumza
Agosti 13 mwaka huu kwenye mtaa wa Kairo Mji mdogo wa Mirerani Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara katika mazishi ya Msuya yaliyohudhuriwa na umati
mkubwa wa watu kutoka mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro, Malongo alisema
Serikali haiwezi kukaa kimya katika suala hilo la mauaji.
Alisema
wafanyabiashara aina ya Msuya wanapouawa pia uchumi nao unaondolewa kwani
wanaiingizia mapato Serikali kutokana na biashara wanazozifanya kwani wanalipa
kodi Serikalini.
Alidai kuwa
kuanzia wiki ijayo, wanatarajia kuwafikisha mahakamani mtandao wa watu
wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara huyo bilionea ambaye amezikwa
jana katika mazishi ya kifahari.
“Nimeongea na
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele ili akutane na wafanyabiasha
na wachimbaji wa madini ya Tanzanite ili matukio ya mauaji yanayotokea kila
mara yaweze kukomeshwa,” alisema Malongo.
Kwa upande wake,
Naibu Waziri huyo Masele aliwatia moyo wachimbaji na wafanyabiashara wa madini
ya Tanzanite kwa kushirikiana katika kipindi hiki kigumu kwani Mungu ndiye
atakayelipiza kisasi hicho cha Msuya.
Naye,Mbunge
wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka amewataka wachimbaji na
wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite kushukuru kwa kila jambo ila mtandao huo
wa kuondoa roho za watu zisizo na hatia ukomeshwe.
“Biblia
inasema tazama ilivyo vema na kupendeza ndugu wanapokutana karibu na kuwa
pamoja hivyo kama mkuu wa mkoa wa Arusha alivyosema kazi ya vyombo vya dola ni
kumaliza ukatili tusiwe na shaka” alisema Ole Sendeka.
Subscribe to:
Posts (Atom)