Mwenyekiti wa CCM Mkoani Manyara, Lucas Ole Mukus akimkabidhi mkurugenzi wa kituo cha wagonjwa na wasiojiweza wa Bashay Wilayani Mbulu Padri James Amnaay, mche wa sabuni kwa ajili ya kituo hicho pamoja na vyakula,nguo na sabuni vilivyotolewa na Jumuiya ya UWT Wilayani Mbulu katika wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa chama hicho. 
Viongozi wa Jumuiya ya UWT Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, wakipanda mti kwenye shule ya sekondari Bashay, kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa CCM.
Friday, 3 February 2017
DC SIMANJIRO AWAASA WANANAISINYAI KUSHIRIKIANA NA TANZANITEONE
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Naisinyai kuhusiana na mahusianao mema na wawekezaji majirani zao kampuni ya TanzaniteOne.
Ofisa mahusiano wa kampuni ya TanzaniteOne, Khalfan Hayesh akisoma mikakati ya kusaidiana kati yao na wananchi wa Kijiji cha Naisinyai, kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Robert Grafen Greaney.
Wednesday, 25 January 2017
MAPADRI WATOA MSAADA KWA WANAFUNZI TARAFA YA EYASI
Padri Miguel Lozano akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Mang'ola Wilayani Karatu Mkoani Arusha, baada ya kutoa msaada wa vitabu 3,000 vya thamani ya shilingi milioni 30 akishirikiana na Padri Pepe.
Padri Miguel Lozano akigawa miongoni mwa vitabu 3,000 vyenye thamani ya shilingi milioni 30 akishirikiana na Padri Jose Torner Pepe wote wa shirika la Roho Mtakatifu Parokia ya Mangola kwa wanafunzi wa shule nne za sekondari za serikali Tarafa ya Eyasi Wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Padri Miguel Lozano akigawa miongoni mwa vitabu 3,000 vyenye thamani ya shilingi milioni 30 akishirikiana na Padri Jose Torner Pepe wote wa shirika la Roho Mtakatifu Parokia ya Mangola kwa wanafunzi wa shule nne za sekondari za serikali Tarafa ya Eyasi Wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Thursday, 12 January 2017
MAPADRI WA MANG'OLA
Mapadri wa Mang'ola walivyoisaidia jamii kiroho na kimwili
Na Joseph
Lyimo
Kwa
asili yake Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana na Mungu. Ni nchi yenye
rasilimali nyingi inayokaliwa na wananchi wanaounganishwa na utaifa wao na kwa
hiyo kuendelea kuwa nchi yenye amani ya kudumu na hivyo kuwa nchi yenye
kuaminiwa na kutumainiwa.
Wananchi
wanaipenda nchi yao na majirani na nchi rafiki wanaipenda Tanzania. Tatizo ni
kwamba yewezekana wengi wetu hatuujui ukweli huo na ikiwa
tunaijua,
basi tunadeka na ama hatutambui uhalisia kwamba unapopendwa na wewe upendeke.
Ukipendwa leo nawe ukakataa kupendwa, kesho ukipenda wewe, utakataliwa na
hutapendwa.Kupendwa ni bahati na siyo haki ya kudaiwa popote!
Nchi
yetu inazo nchi rafiki ambao zina urafiki wa kinafiki lakini pia inazo nchi
rafiki ambazo ni marafiki wa kweli na wanaoitakia nchi yetu mema kupitia
wananchi wao wanaokuja kutembelea nchi yetu, kuwaona watu na mifumo yao ya
kijamii, maisha yao na changamoto zao.
Wapo
pia wanaokuja kuona rasilimali na fursa za uwekezaji. Pia, wapo watu binafsi
kutoka nchi hizo rafiki, ambao huguswa na changamoto za watu wetu nao huingiwa
na ukarimu wa kutaka kutusaidia kuondokana na changamoto hizo.
Tanzania
imebahatika kupendwa kwa dhati kwa takriban miaka 40 sasa yaani tangia Mwaka
1976 na mapadri wawili Jose Aguilar Torner na Miguel Angel Lozano ambao ni wa Shirika
la Roho Mtakatifu kutoka nchini Hispania.
Mwananchi
wa Kijiji cha Narakauwo Kata ya Loiborsoit Tarafa ya Emboreet Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara, Lucas Ole Mukusi ambaye aliwahi kuwa diwani wa kata
hiyo na hivi sasa ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo anasema kwa mara ya kwanza mapadri
hao kufika kwao Tanzania walipewa kituo cha kazi Parokia ya Emboreet, katika
mbuga za Tukutta.
Ole
Mukusi anasema mapadri hao wawili walifanya kazi kubwa parokiani hapo kwa
kujenga majengo ya kuishi mapadri na masista, majengo ya kutolea huduma ya uhakika
ya afya, zahanati yenye kutoa huduma ya wagonjwa wa nje OPD na pia kulaza
wagonjwa, vitanda 30, huduma ya afya ya mkoba, huduma ya afya ya uokoaji kwa
njia ya ndege (Flying Doctors Service) na kuimarisha huduma ya maji kutokea
kwenye chanzo hadi katika shule ya Msingi na kupanua mtandao hadi kituo cha
Afya.
Anasema mapadri hawa walifanya kazi Emboreet
Simanjiro hadi mwaka 1983 ambapo Padri Jose Aguilar Torner (maarufu kwa jina la
Pepe) alipohamia Engikaret-Monduli na PadrI Miguel Angel Lozano (Maarufu kwa jina
la Oloronyo) akahamia Loliondo-Ngorongoro mnamo mwaka 1985.
Anaeleza
kuwa huko Engikaret, padri Pepe alijenga nyumba za kuishi mapadri na masista,
kuboresha shule ya makatekista kuwa sekondari kwa majengo na vifaa vya
kufundishia, kujenga kanisa na zahanati ambako huduma bora na ya uhakika ya
afya ilitolewa kwa mara ya kwanza.
“Wakati
wote huo, dawa nyingi na vifaa vya kisasa vililetwa kutoka Hispania na mara kwa
mara wataalamu wabobezi wa maradhi mbalimbali walifika kutoa huduma za rufaa
kwa wagonjwa wa maeneo walikofanya kazi mapadri hao na kwa njia hii, maisha ya wagonjwa
wengi yaliweza kuokolewa,” anasema.
Anaongeza
kuwa mwaka 1993, mapadri hawa walikutanishwa tena ili kufanya kazi pamoja,
baada ya askofu wa Jimbo la Arusha, kuwatuma kwenda eneo la Mang’ola Chini ili
kuchochea maendeleo ya kiroho na kimwili jambo ambalo wamelifanya kwa takriban
miaka 23 kwa ufanisi mkubwa mno.
Anasema
mapadri hao wawili Pepe na Miguel ni wabunifu mno na viongozi wenye moyo mkuu
katika kuwahudumia watu wao bila kujali imani ya jamii ya maeneo ambako wanatoa
huduma ya kiroho.
Huduma
za kitaalamu za afya na mambo mengine.
Mapadre
wa Mang’ola-chini, Pepe na Miguel ni watu ambao daima hufikiria njia za
kupambana na matatizo yanayowakabili watu wao, katika kufanya hivyo, hukabiliwa
na changamoto za ubabe na ukorofi wa baadhi ya viongozi na wanasiasa wenye
mwelekeo usiokuwa na manufaa kwa jamii ya Mang’ola na Tanzania kwa ujumla wake,
jambo ambalo huwawia vigumu mapadri hawa kukubaliana nalo.
Ole
Mukusi anasema katika kuboresha utoaji wa huduma za kiafya, mapadri hawa
wamejenga mahusiano na mashirika yenye kutoa huduma kwa mfano wataalamu wa
meno, mifupa na masikio kutoka nchi ya Hispania.
Anasema
wataalamu hawa huja kwa makundi yenye kutofautiana kwa ukubwa na kipindi cha
kuja Mang’ola na idadi ya wataalamu katika makundi haya ni kuanzia watu nane
hadi 16 na kwamba wanayapokea makundi matatu hadi manne kwa mwaka.
“Licha
ya kuwa CBO ya WAVIU inalo Trekta, ambalo hulitumia kukodishia wakulima ili
kupata fedha, mapadre huwapatia WAVIU huduma ya afya bure pamoja na chakula, mapadre
hao wameanzisha CBO kwa ajili ya jamii ya Wahadzabe katika kuwasaidia waweze
kupata mahitaji ya muhimu ya kibinadamu, kupitia utalii unaofanywa katika
maeneo yao,” anasema.
Anasema
kuwa mapadri hao wamewezesha uanzishaji wa shule mbili za awali kwa nia ya
kuunga mkono juhudi za serikali za kuwapatia watoto wa wananchi wa Mang’ola elimu.
Anasema
kwa nyakati ambazo wataalamu wa huduma za rufaa kutoka Ulaya hawapo, kila inapolazimu
mgonjwa anahitaji huduma ya dharura, gari la wagonjwa humsafirisha mhusika
kwenye huduma Arusha au KCMC Mkoani Kilimanjaro na mara zingine Dar es salaam.
Anasema
mapadri hao wamejenga mahusiano na shirika la La Arruzafa Foundation yenye makao
yake Cordoba Hispania ambayo hufanya huduma mbalimbali za macho, ambapo wataalamu
kutoka taasisi hiyo walifika Mang’ola mwaka jana na kwa wiki moja walihudumia
wagonjwa wa macho 736 kati yao wagonjwa 600 walipewa miwani ya thamani kati ya
sh65,000 na sh90,000 ya kuonea, kusomea na ya kukinga mionzi mikali ya jua.
Anasema
upasuaji mkubwa ulifanyika mara 74 na zote zilifanyika vizuri na kwa muda wote huo,
La Arruzafa Foundation iliwalipa watumishi wa kituo cha afya Mang’ola, posho
zao za siku na zile za ufanyaji kazi wa ziada na kuwapatia huduma za chakula na
malazi wagonjwa wasio na uwezo wa kujikimu au kujihudumia malazi na chakula.
“Upasuaji
huo ulifanyika katika chumba cha upasuaji iliyosheheni vifaa vingi vya kisasa
ambavyo wataalamu hao hupenda kushirikiana na wataalamu wetu wa wilaya na mkoa
ili kuwajengea uzoefu katika matumizi ya vifaa hivyo,” anasema na kuongeza;
“Hata
hivyo, kuna hofu kuwa wanafunzi wengi wa Mang’ola wanakabiliwa na uoni hafifu
nyakati za giza kutokana na hali ya kijiografia na hivyo kuwa sababu ya
wanafunzi wengi kupatiwa miwani ya kupunguza ukali wa mionzi mikali ya jua.”
Anasema
mapadri wamewezesha uanzishaji wa shule mbili za awali kwa nia ya kuunga mkono
juhudi za serikali za kuwapatia wananchi elimu na kwa nyakati ambazo wataalamu wa
huduma za rufaa kutoka Ulaya hawapo, kila inapolazimu
kwamba
mgonjwa anahitaji huduma ya dharura, gari la wagonjwa humsafirisha mhusika
kwenye huduma Arusha au KCMC mkoani Kilimanjaro na mara zingine Dar es salaam.
Jamii
ya Mang’ola yawazungumzia mapadri hao
Mmoja
kati ya wakazi wa eneo hilo Antony John anasema japokuwa suala la kufanikisha
maendeleo ya jamii ikiwemo shule, maji, miundombinu, afya ni jukumu la
serikali, lakini viongozi hao wa dini wamejitahidi kwa uwezo wao kufanikisha
hayo.
“Kutokana
na hali hiyo viongozi hawa wa kiimani wanapaswa kukumbatiwa na kuungwa mkono
kwani kwa muda wote waliokuwa hapa Mang’ola wametuonyesha kuwa wao ni watu wa
maendeleo na wamebadili eneo hili likawa na maendeleo ya kutosha,” anasema
John.
Hamisi
Bakari mkulima wa vitunguu anasema mapadri hao wamekuwa wanatoa msaada kwa
jamii ya eneo hilo bila kubagua dini au madhehebu hivyo serikali inapaswa
kuwapa ushirikiano wa kutosha kupitia maendeleo wanayofanya katika eneo hilo la
Mang’ola.
“Japokuwa
wenyewe ni mapadri wa kanisa katoliki lakini wamefanikisha ujenzi wa msikiti
kwenye eneo letu la Mangola hivyo kuunganisha mioyo ya watu wa madhehebu
mengine na kitendo hicho kimetufanya tuwe ndugu moja japokuwa sisi ni watu wa
imani tofauti,” anasema Bakari.
Rai
kwa Rais John Magufuli
Ole
Mukusi anasema pamoja na ukweli kuwa mapadri hawa wa Shirika la Roho Mtakatifu
wamekuwepo nchini kwa takriban miaka 40 yaani kipindi muhimu cha maisha yao,
hadi sasa bado wanakabiliwa na changamoto ya kupatiwa vibali vya kuishi hapa nchini
ili kuwahudumia Watanzania bila wao kupata faida
yoyote
binafsi.
“Kwa
miaka yote waliyowatumikia watu wetu, bado wanaendelea kama vile ndio wanakuja
leo nchini na kwa hiyo wanapatiwa kwanza visa ya kitalii ili hali mapadre hawa
wanaisaidia serikali yetu katika kutekeleza jukumu la kuihudumia jamii yetu kiroho,
kielimu na kiafya,” anasema.
Anaeleza
kuwa mapadri hawa hupata usumbufu mkubwa kila wanapoomba vibali vya wataalamu
wa afya kuingia nchini ili kutoa huduma ya bure kwa Watanzania.
“Pia
wao huchukua muda mwingi kuvipata vibali hivi ambavyo hulipiwa fedha nyingi
bila hata kujali kwamba wataalamu hawa wanakuja kuokoa bure maisha ya jamii ya
Tanzania,” anasema Ole Mukusi.
Anasema
Mungu anatutumikia kupitia wataalamu hawa na ndiyo sababu
wanaihudumia
Tanzania kwa upendeleo mkubwa kwani wamefanya kazi nchini Benin miaka miwili,
Equatoria Guinea miaka mitano, Madagascar miaka saba na Tanzania miaka 11 na bado
wana nia na moyo wa kuendendelea kutoa huduma.
“Hapa
kwetu, wanawapatia jamii huduma zao bure kwa kutumia vifaa walivyotoa kama
msaada pamoja na kwamba vipo vingine ambavyo wanakuja navyo na kurudi navyo
kutokana na kwamba watu wetu hawana taaluma ya kuvitumia,” anaeleza.
“Rais
wetu Dk John Magufuli ni mtu mwenye moyo wa huruma na shukrani, mwenye kutambua
na kuthamini kazi nzuri inayofanywa, ndiyo sababu yake ya kutumia Kauli Mbiu ya
‘hapa kazi tu’ namuomba Rais wetu mpendwa atembelee Mang’ola ili apate kujionea
kwa macho yake mwenyewe kazi na historia njema ya ufanisi inayofanywa na
mapadri hawa,” anasema na kuongeza;
“Ninaiomba
Serikali yetu ifanye marekebisho ya kimfumo ili kurahisisha mchakato wa
upatikanaji wa vibali kwa watu wa mataifa mengine wenye nia njema ya kuisaidi
nchi yetu.”
Anasema
kupitia kwa viongozi hao wa dini wamefanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo
kwenye eneo la Mang’ola yenye thamani ya sh5,973,661,000 ikiwemo ujenzi wa
madarasa 40 ya shule za msingi zilizotumia sh400.5 milioni, ujenzi wa Nyumba 35
za walimu sh350.7 milioni, ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana sh2.3
milioni, ujenzi wa ukumbi na ofisi nne za vijiji na nne za kata sh85 milioni.
Anasema
ukarabati wa shule 11 za msingi kwenye Tarafa ya Mang’ola sh301.5 milioni,
ujenzi wa Kituo cha afya sh1.2 bilioni, ufadhili wa fedha za uendeshaji wa
kituo cha afya kila mwaka sh160.6 milioni, kukarabati kituo cha polisi sh3.1
milioni na kuchangia ujenzi wa msikiti sh25.8 milioni.
Pia,
wamefanikisha ujenzi wa nyumba tano za watu wasiojiweza kwa gharama ya sh25
milioni, ununuzi wa trekta na vifaa vyake kwa CBO ya WAVIU sh62.8 milioni, kuhudumia
kikundi cha wazee, wajane na wagane 25 sh23.4 milioni na kujenga ukumbi na
bwalo la magereza sh25 milioni, ununuzi wa vitabu vya shule za msingi Tarafa ya
Mangola sh75.3 milioni.
Anasema
wamefanikisha ununuzi wa madawati kwa shule za msingi kwenye tarafa hiyo sh75
milioni, ujenzi wa mradi wa maji ambapo kuna mtandao wa miundombinu wenye
umbali wa Kilometa saba sh300.7 milioni, ununuzi wa vitabu vya shule nne za
sekondari kwa mwaka 2016 sh30.1 milioni, ujenzi wa kanisa katoliki lenye uwezo
wa kuingia watu 1,500 sh1.800 bilioni.
“Pia
kuna ujenzi wa makanisa matano katika vigango sh250.5 milioni, ujenzi wa kituo
cha masista wafanyao kazi za afya na shuleni sh180.6 milioni, ujenzi wa
karakana ya mafunzo ya useremala kwa vijana sh21.9 milioni, ununuzi wa vifaa
katika karakana ya useremala sh200.6 milioni,” anasema Ole Mukusi.
Anasema
pia ujenzi wa Kituo cha mafunzo kwa wasichana sh62.9 milioni, ujenzi wa maghala
12 ya kuhifadhia vitunguu katika vijiji saba sh180.8 milioni, kuwasomesha
vijana 55 chuo kikuu sh125.9 milioni, vyote vimegharimu zaidi ya sh5.9 bilioni,
ikiwa ni michango ya watu wa Hispania kwa watanzania muda ambao mapadre hao
wamefanya kwenye parokia yao Mang’ola.
Anasema
kwa muda waliofanya kazi Parokia ya Mang’ola mapadre hao Pepe na Miguel
wamewezesha miradi hiyo iliyogharimu fedha hizo shilingi 5,973,661,000 ambayo ni michango ya watu wa Hispania kwa
Watanzania waliopo Tarafa ya Mang’ola.
KAMPENI YA UDIWANI KATA YA DURU BABATI
Mgombea udiwani wa Kata ya Duru Wilayani Babati Mkoani Manyara, Jackson Haibei (CCM) akizungumza jana wakati akijinadi na kuomba kura kwa wananchi wa Kijiji cha Hoshan.
LOSOITO WAPATIWA MAJI NA TANZANITEONE
Kaya
277 za wananchi 1767 wa Kijiji cha Losoito, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,
wenye tatizo kubwa la ukosefu wa maji, wanatarajia kuondokana na changamoto
hiyo baada ya kampuni ya TanzaniteOne kuwapatia maji.
Ofisa mahusiano
wa kampuni ya madini ya Tanzanite ya wilayani humo TanzaniteOne Halfan Hayeshi
akizungumza alisema hivi sasa mradi huo umefikia asilimia 85 ili umalizike
na kuzinduliwa ila wanachi wanapata maji.
Hayeshi alisema
wananchi wa eneo hilo wanaendelea kupata huduma ya maji ila mradi kamili
haujakamilika kwani wanahitaji kuweka mabomba urefu wa mita 500 ili kufikisha
maji hayo karibu zaidi na jamii eneo la shule ya msingi Losoito.
“Tunatarajia
kuweka mabomba ya urefu wa mita 500 ili kufikisha mradi huu karibu zaidi, ila
hivi sasa wananchi wanapata huduma hiyo ya maji kwani awali tuliambiwa
tufikishe mradi huo kwenye eneo la sasa ulipo,” alisema Hayeshi.
Alisema
wanatarajia kuzindua mradi huo hivi karibuni baada ya kuwapa taarifa Katibu
tawala wa mkoa huo Eliakim Maswi na mkuu wa wilaya hiyo Zephania Chaula, ambao
ndiyo wataukabidhi kwa wananchi wa kijiji hicho cha Losoito.
Alisema mifugo na
jamii ya eneo hilo hivi sasa wanafaidika na huduma hiyo ya maji na mara baada
ya kununuliwa kwa rola sita za mabomba ya maji yatakayoweza kuwekwa katika mita
500 zilizobaki yatafika kwenye shule hiyo.
Ofisa mtendaji wa
kijiji hicho Ngatayai Mollel alishukuru uongozi wa kampuni ya TanzaniteOne kwa
kufanikisha mradi huo wa maji, utakaowasaidia wananchi wa eneo hilo, ambao kwa
muda mrefu walikuwa wanakabiliwa na tatizo la maji.
Mollel alisema
kijiji hicho kilichoanzishwa mwaka 2009 hivi sasa kina wakazi 1767 chenye kaya
277 kilikuwa na wakati mgumu wa kupata huduma ya maji ila hivi sasa wananchi wameondokana
na changamoto ya maji iliyowasumbua.
Hata hivyo,
alitoa ombi la wananchi wa eneo hilo kujengewa zahanati kwani inawalazimu
kutembea umbali mrefu kupata huduma ya afya pindi wanapougua hivyo kuwa tatizo
hasa kwa wanawake na watoto.
Mmoja kati ya
vijana wanaolinda mradi huo wa maji ili mabomba yasiibiwe Daniel Solomon, alisema
wamepeana zamu ya kulinda kila siku watu watatu ili miundombinu isiharibiwe na
jamii ya eneo hilo ifaidike na maendeleo hayo.
“Wakina mama
walikuwa wanatembea umbali mrefu wa kilomita 20 kila siku kwenda na kurudi mji
mdogo wa Mirerani, kwa kutumia wanyamakazi punda, ila hivi sasa wanaondokana na
tatizo hilo la muda mrefu,” alisema Solomon.
Tuesday, 20 December 2016
VODACOM YATOA MSAADA KITUO CHA WAZEE SARAME MAGUGU BABATI MANYARA
Meneja
ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald,
akimkabidhi, mmoja kati ya wazee wa kituo cha wazee na wasiojiweza
Sarame Magugu, Wilayani Babati Mkoani Manyara, Maalim Masaja chandarua,
ambapo waliwakabidhi wazee hao mashuka, vyandarua, vyakula, dawa na
mahitaji mengine yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni.
Meneja
ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald,
akimkabidhi Khadija Omari, mmoja kati ya wazee wa kituo cha wazee na
wasiojiweza Sarame Magugu, Wilayani Babati Mkoani Manyara, shuka na
vyandarua, baada ya kukabidhi msaada wa vyakula, dawa na mahitaji
mengine yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni.
TUZO UTUNZAJI MAZINGIRA
Mkuu wa Babati ya Babati Raymond Mushi akiwa ameshika tuzo ya utunzaji mazingira aliyokabidhiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera
Mkuu wa
Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akiwa amemkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa huo Eliakim Maswi tuzo ya utunzaji mazingira
Saturday, 17 December 2016
WATAKIWA KUONDOA MIGOGORO MANYARA
Mkuu wa
Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera amewataka viongozi wa Wilaya kuhakikisha
wanashirikiana ipasavyo ili kutatua migogoro ya ardhi inayorudisha nyuma
maendeleo kwani robo tatu ya mkoa huo imegubikwa na migogoro.
Dk Bendera
akizungumza mjini Babati kwenye mafunzo elekekezi kwa viongozi wa wilaya
za mkoa huo alisema, migogoro ya ardhi kwa kiasi kikubwa ndiyo kikwazo cha
maendeleo hivyo watumie uwezo wao wote ili kuimaliza.
Alisema kila
kiongozi kwa nafasi yake anapaswa kuhakikisha anasimama vyema katika kutekeleza
majukumu zaidi kwani migogoro mingi inaweza kumalizika endapo itatiliwa maanani
kwenye utekelezaji ili kupiga hatua ya maendeleo.
Alisema migogoro
ya ardhi ambayo imetawala kwenye robo ya sehemu ya Manyara inapaswa kumalizika
kwa kuhakikisha viongozi wote wa wilaya wanawajibika kumaliza migogoro hiyo
isiyokuwa na faida yoyote.
“Tunapaswa
kutimiza wajibu wetu ipasavyo kwa kuhakikisha viongozi wa kisiasa na watendaji
wanatumia nafasi zao kikamilifu ili kumaliza migogoro hiyo ambayo haina manufaa
kwa wananchi tunaowaongoza,” alisema Dk Bendera.
Mkuu wa wilaya ya
Kiteto Tumaini Magessa, alisema matatizo mengi ya mkoa wa Manyara kuhusu
migogoro hiyo ni kutokuwepo kwa matumizi bora ya ardhi kwani wilaya hiyo
imetumia miaka 10 kusuluhisha migogoro na haijamalizika.
“Wilaya yetu imetumia
miaka mingi mno kwa ajili ya kusuluhisha migogoro ili hali tungeweza kutumia
muda huo kwa ajili ya kujenga madarasa, shule na kufanya maendeleo mengine
hivyo tunapaswa kubadilika,” alisema Magessa.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Yefred Mnyenzi alisema inapaswa
sheria, taratibu na kanuni (STK) zifuatwe katika utekelezaji kwani kuna baadhi
ya watu wanamilikishwa ardhi bila kufuata utaratibu halali.
Mkuu wa wilaya ya
Simanjiro Zephania Chaula alisema viongozi wa wilaya yake na wilaya ya Kiteto
watakutana hivi karibuni ili kusuluhisha mgogoro wa ardhi uliopo kwenye kata ya
Emboreet Simanjiro na kata ya Makame Kiteto.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Tamimu Kambona alisema wanakabiliwa
na migogoro mingi ya mipaka kwenye wilaya jirani ikiwemo Kilindi, Gairo, Chemba
na Simanjiro hivyo mkoa ushiriki kuitatua.
Subscribe to:
Posts (Atom)




