Thursday, 29 May 2014
Wednesday, 28 May 2014
KINANA AINGIA MANYARA
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mkoani
Manyara, alipoanza ziara yake wilayani humo (kushoto) ni Katibu wa CCM Mkoani
humo, Ndengasso Ndekubali na katikati ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoani humo,
Fratey Massey na aliyekuwa Waziri Mkuu, Fredrick Sumaye.
Katibu
Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye akisalimiana na na Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mkoani
Manyara, ambapo yeye na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahaman Kinana, walipoanza ziara yao wilayani humo katikati ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoani humo,
Fratey Massey
Monday, 26 May 2014
UCHAGUZI MARA GROUP
Jamii
ya Mara Group ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,
wakiwa wamembeba Mwenyekiti wao, Philemon Oboro aliyechaguliwa jana kwa kupata kura 523 hivyo
kuongoza jamii hiyo.
amii ya Mara Group ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa wamembeba Makamu Mwenyekiti wao, Elija Ambonya aliyechaguliwa jana kwa kupata kura 363 hivyo kuongoza jamii hiyo.
amii ya Mara Group ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa wamembeba Makamu Mwenyekiti wao, Elija Ambonya aliyechaguliwa jana kwa kupata kura 363 hivyo kuongoza jamii hiyo.
Jamii
ya Mara Group ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,
imemchagua Philemon Oboro, kuwa Mwenyekiti wake kwa kipindi cha miaka mitatu
baada ya kuwaangusha wapinzani wake watatu.
Akitangaza
matokeo hayo jana, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi huo Samwel Ombeng alisema
Oboro alipata kura 523, Philipo Mtanda Onyando kura 60, Allan Gichana kura 33
na Jackson Onyango Mutaban kura nane.
Ombeng
alisema Elija Ambonya alichaguliwa kuwa Mwenyekiti Msaidizi kwa kupata kura 363
na kumshinda Thobias Magati aliyepata kura 305 na Stephen Odoya, alichaguliwa
kuwa Mweka hazina, baada ya kukosa mpinzani.
Naye,
katibu wa tume hiyo Gerald Orinya (Team Coach) alisema Elija Ambonya alichaguliwa kuwa
Katibu wa Mara Group kwa kupata kura 363 na kuwashinda Adam Wambura kura 117,
Msafiri Marwa kura 130 na Omenda Odero kura 84.
Orinya
alisema George Okwaro alishinda nafasi ya Katibu msaidizi kwa kupata kura 378
na kumshinda Samwel Orafa aliyepata kura 221 na Asubuhi Kibaso alishinda nafasi
ya Kamanda wa Mara Group, baada ya kupita bila kupingwa.
Katibu
wa Utegi kaskazini, Atanas Ongati (Power Tiler) alisema lengo la Mara Group ni
kusaidiana kwenye shida na raha na kuhakikisha watu wote wanaofariki wakiwa
Mirerani wanasafirishwa na kwenda kuzikwa nyumbani kwao mkoani Mara.
Akizungumza
baada ya kuchaguliwa, Oboro alisema atawaongoza ipasavyo wana kikundi hao bila
ubaguzi na dhamira yake ni kuwaunganisha pamoja kwa kutojali waliompigia kura
au wasiompigia kwani wote ni wamoja.
Naye,
Mwenyekiti msaidizi Ambonya alisema kupitia ushirikiano walionao watahakikisha
Mara Group inazidi kuimarika na kusaidiana na jamii yote ya mji mdogo wa
Mirerani bila kujali tofauti, kwani ushirikiano ndiyo nguzo ya umoja.
Thursday, 22 May 2014
WAJUMBE WA HALMASHAURI YA CCM BABATI MJINI
![]() |
| Diwani wa kata ya Bonga Mjini Babati Mkoani Manyara, Pasian Siay akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM ya wilaya ya Babati. |
![]() |
| Katibu wa CCM wa Mkoa wa Manyara, Ndengasso Ndekubali akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri ya wilaya ya Babati mjini. |
![]() |
| Wajumbe wa Halmashauri ya CCM Babati mjini Mkoani Manyara wakifuatilia kikao cha Halmashauri ya wilaya hiyo. |
ZIMAMOTO
![]() |
| Mwanafunzi wa shule ya msingi Babati Mkoani Manyara wakipatiwa elimu ya zimamoto na uokoaji wakati askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji Manyara walipokuwa wanatoa elimu ya zimamoto shuleni hapo |
![]() |
| Wanafunzi wa shule ya msingi Babati Mkoani Manyara wakipatiwa elimu ya zimamoto na uokoaji, wakati askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji Manyara walipokuwa wanatoa elimu ya zimamoto shuleni hapo |
WACHIMBAJI MADINI TANZANITE
![]() |
| Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani |
![]() |
| Diwani wa Kata ya Endiamtu Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini |
![]() |
| Wanachama wa CCM na wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakimpokea Mbunge wa Jimbo hilo Christopher Ole Sendeka |
MJASIRIAMALI
WAUGUZI HANANG
![]() |
| Wauguzi wa Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara wakiandamana wakati wa kuadhimisha siku ya wauguzi duniani ambapo wao walichelewa kufanya Mei 12 kutokana na kuwa na wagonjwa wengi |
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Hanang Christina Mndeme akizungumza na waguzi wa wilaya hiyo |
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Hanang Christina Mndeme akizungumza na waguzi wa wilaya hiyo |
Wednesday, 21 May 2014
TUNAPASUA KUNI
Baadhi ya
wanafunzi wa shule ya sekondari Measkroni Wilayani Hanang Mkoani Manyara,
wakipasua kuni za kupikia chakula shuleni hapo
Subscribe to:
Posts (Atom)















