Sunday, 27 April 2014

MAHAFALI YA SHULE YA SEKONDARI DR OLSEN



Wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne wametakiwa wasiridhike na elimu waliyoipata hivyo wajiendeleze zaidi kwenye vyuo mbalimbali kwa manufaa yao ya baadaye kwani kuhitimu elimu hiyo siyo mwisho wa kusoma.
Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Ofisa Elimu wa mkoa wa Manyara, Ibrahim Mbang’o kwenye mahafali ya tano ya kidato cha sita kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Dr Olsen iliyopo Wilayani Mbulu.
Mbang’o alisema hatua waliyofikia ni mwandelezo wa safari ya taaluma hivyo kuhitimu siyo mwisho wa elimu ila wanatakiwa kupiga hatua nyingine na kuhakikisha wanafaulu mitihano yao na kuingia chuo kikuu.
“Hatua mliyofikia ni kubwa hivyo jiendelezeni zaidi na msikubali kuolewa au kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na ulevi jamani someni na kufikia hatua ya juu zaidi” alisema Mbang’o.
Alisema watumie elimu waliyoipata kwa kujiendeleza zaidi na aliwapongeza kwa kufikia hatua hiyo kwani walijilisha na kujiepusha na tamaa na kutawala nafsi zao, vishawishi na anasa nyingine.



 Mwanafunzi wa kidato cha sita wa shule hiyo, Jackline Nanyaro akionyesha namna ya kumpasua panya kwenye somo la baiolojia katika mahafali ya sita ya shule hiyo.
Naye, mkuu wa shule ya Dr Olsen, Ernest Asseri alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1997 ikiwa na kidato cha kwanza na mwaka 2007 ilianzishwa kidato cha tano na sita kwenye michepuo ya PCB na CBG.
Asseri alisema hadi hivi sasa wana wanafunzi 22 wa kidato cha sita wanaotarajia kufanya mtihani wa kidato cha sita May 5 mwaka huu na wanatarajia kufaulisha wanafunzi wengi kwenda vyuo vikuu.
Alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mdondoko na utoro kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne, upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwa kidato cha tano na sita.   

NASOMA RISALA


Mkuu wa shule ya sekondari Dk Olsen ya Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Ernest Asseri akizungumza katika mahafali ya kidato cha sita yaliyofanyika jumamosi iliyopita shuleni hapo.

Monday, 21 April 2014

PASAKA ILIVYOSHEREHEKEWA MJI MDOGO WA MIRERANI


Wanakwaya wa Mtakatifu Cecilia wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozali Takatifu wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiimba baada ya kumaliza misa ya Pasaka kanisani hapo jana.


Padri Modestus Makiluli, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozali Takatifu wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,akiendesha misa ya ubatizo na komuniyo kwenye kanisa hilo wakati wa sikukuu ya Pasaka, Aprili 20.



Bwana harusi Ladslaus Manyanya (kulia) na mkewe Patricia Magero, (wa pili kulia) wakiwa na wapambe wao baada ya kufunga ndoa jana kwenye sikukuu ya pasaka katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozali Takatifu wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Familia ya Kalacheni, ikiwa na furaha baada ya kumaliza kusali sikukuu ya pasaka kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozali Takatifu wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

IJUMAA KUU



Waumini wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozali Takatifu, wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakishiriki ibada ya Ijuma Kuu kwenye kanisa hilo.


Sunday, 20 April 2014

SIKU YA MKULIMA WA UFUTA BABATI


Wasanii wa Goroa Tradition Dancing group wa Kata ya Qash Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakitoa burudani kwa wadau wa zao la ufuta, kwenye siku ya mkulima iliyofanyika kitongoji cha Maweni, Kijiji cha  Endadosh, Kata ya Qash, Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
 Afisa kilimo wa mradi wa ufuta wa shirika la Farm Africa, Tumaini Elibariki akimsikiliza Mtafiti wa Biosciences for Farming in Africa, kutoka London Uingereza, Claudia Canales kwenye siku ya mkulima iliyofanyika katika kitongoji cha Maweni, Kijiji cha Endadosh, Kata ya Qash, Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

Wasanii wa Goroa Tradition Dancing group wa Kata ya Qash Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakitoa burudani kwa wadau wa zao la ufuta, kwenye siku ya mkulima iliyofanyika kitongoji cha Maweni, Kata ya  Endadosh Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.


Wadau wa kilimo cha ufuta wakiwa kwenye siku ya mkulima wa ufuta iliyofanyika kwenye kitongoji cha Maweni, Kitongoji cha Endadosh, Kata ya Qash Wilayani Babati Mkoani Manyara.


Mkulima wa zao la ufuta katika Kitongoji cha Maweni, Kijiji cha Endadosh, Kata ya Qash, Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, John Kunda, akiwaelezea Ofisa kilimo wa huo, Coletha Shayo na Ofisa kilimo wa mradi wa ufuta wa Shirika la Farm Africa, Tumaini Elibariki namna alivyoliendeleza shamba lake la ufuta