Saturday, 21 December 2013

AJALI BASHNET



Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Manyara na baadhi ya wakazi wa Bashnet wakiwa kwenye eneo la tukio la ajali ya gari lililokuwa limebeba mahindi na kuanguka kwenye mlima wa Bashnet Wilayani Babati.



Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Manyara wakiwa katika eneo la tukio la ajali ya gari lililokuwa limebeba mahindi na kuanguka kwenye mlima wa Bashnet Wilayani Babati, ambapo ajali ilikuwa mbaya ila hakuna aliyepoteza maisha kwenye gari hili lililokuwa na watu wawili yaani dereva na kondakta wake.



Jamani wamepona ehee? Baadhi ya wakazi wa eneo la Bashnet wakitazama ajali ya gari ambapo dereva alikimbia baada ya ajali hiyo.

MADIWANI MBULU



Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara

Friday, 20 December 2013

HONGERA SANA


Mkuu wa Kituo cha polisi Mirerani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Ally Mohamed Mkalipa (kushoto) akimpongeza aliyekuwa Ofisa utumishi wa wilaya hiyo, Patrice Saduka aliyehamishiwa wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani, kwenye tafrija ya kumuaga iliandaliwa na watendaji wa kata za Simanjiro

NDEGE YA ETHIOPIA



Abiria 213 waliokuwa wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia jana walinusurika kifo baada ya ndege hiyo kutua kwa dharura katika uwanja mdogo wa Arusha.
Ndege hiyo aina ya Boeing 767, ilitua saa 6.45 mchana katika uwanja huo baada ya kushindwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) kutokana na kupata pancha kwa ndege nyingine inayomilikiwa Shirika la Ndege la Tanganyika (TFC), kwenye njia ya uwanja huo.
Ndege ya Ethiopia ililazimika kuelekea Arusha na kutua kwenye uwanja huo mdogo kuweza kupokea ndege kubwa kutokana na kuishiwa mafuta.



Ndege hiyo iliyokuwa inatokea Addis Ababa, Ethiopia ikiwa pia na wahudumu 23, baada ya kutua kwenye Uwanja wa Arusha, ilinasa kwenye tope baada ya tairi lake la mbele kuvuka sehemu ambayo lami inaishia kutokana na ufupi wa njia zinazotumiwa na ndege zinapotua kwenye uwanja huo.
Jitihada za kuiondoa ndege hiyo zilishindikana Desemba 18. Ndege hiyo ilikuwa ikielekea Johannesburg, Afrika Kusini kwa kupitia Kia na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema: “Rubani amejitahidi kutua katika uwanja huu japo ni mdogo ili kuokoa maisha ya abiria kwani walikuwa hawana mafuta ya kutosha kwenda uwanja mwingine.”
Tukio la ndege hiyo kutua kwa dharura limekuja siku chache tangu ndege ya Shirika la Ndege la Precision iliyokuwa na abiria 37 kupasuka matairi manne ilipokuwa ikitua kwenye Uwanja wa KIA Jumamosi iliyopita.