Sunday, 5 May 2013

MLIPUKO OLASITI ARUSHA


Kanisa Katoliki Parokia ya Olasiti jijini Arusha ambapo kulitokea mlipuko leo asubuhi

Kanisa Katoliki Parokia ya Olasiti jijini Arusha ambapo kulitokea mlipuko leo asubuhi

Baadhi ya majeruhi kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Olasiti jijini Arusha ambapo kulitokea mlipuko leo asubuhi

Thursday, 2 May 2013

BWAWA LANGAI



Diwani wa kata ya Langai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Jackson Sipitek akiwaonyesha baadhi ya wakazi wa eneo hilo sehemu ya bwawa lililoharibika.

Tuesday, 12 March 2013

WANAAPOLO WA TANZANITE



Hawa ni wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite (WanaApolo) wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambao ni kati ya zaidi ya Watanzania milioni moja wanaotegemea uchimbaji mdogo wa madini na inakadiriwa kuwa madini ya Tanzanite huingiza mapato yanayofikia dola za marekani milioni 20 kwa mwaka hapa nchini lakini soko la dunia takwimu zinaonyesha huwa mauzo ya dola milioni 500 za marekani kwa mwaka yanafanyika,kiasi ambacho ni kikubwa mno ukilinganisha na takwimu za mauzo zinazopatikana hapa nchini.

ZIARA YA KINANA CHINA



Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Khadija Aboud akisalimiana na  Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC),Huang Xianyao,Aboud alikuwa kwenye msafara wa viongozi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahaman Omary  Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,China.



Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Omary Kinana akimkabidhi zawadi ya kinyango cha Kimakonde,  Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao,  Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,China.