Thursday, 17 August 2017
Tuesday, 1 August 2017
DC AZINDUA KAMPENI YA KUPIMA UJAUZITO
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara,
Chelestino Mofuga amezindua kampeni ya kuwapima ujauzito wanafunzi wa shule za
msingi na sekondari Wilayani humo kwa lengo la kupiga vita watoto wa kike
kupata mimba mashuleni.
Akizungumza wakati kuzindua zoezi hilo,
Mofuga alisema kauli mbiu ya Mbulu bila mimba za wanafunzi na tuache watoto wa
kike wasome inapaswa kutekelezwa kwa vitendo.
Alitoa agizo kwa mkurugenzi wa mji wa Mbulu
Anna Mbogo, mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga na
maofisa elimu kuhakikisha wanaendesha zoezi la upimaji mimba kila baada ya
miezi mitatu.
Alisema huo ni utekelezaji wa agizo la Rais
John Magufuli alilolitoa hivi karibuni ili kuhakikisha hakuna wanafunzi
wajawazito na waliozaa watakaoendelea na masomo katika mfumo wa kawaida.
"Natoa onyo kwa baadhi ya walimu na
wananchi makatili wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi kwani
watapata adhabu kali ya kwenda jela miaka 30 na kazi ngumu kwani hili limeshazungumzwa
na Rais Magufuli," alisema Mofuga.
Aliwataka wakuu wa shule za sekondari na
walimu wakuu wa shule za msingi kusimamia taaluma na nidhamu na kuwafichua
wazazi na walezi wanaoficha wahalifu wanaowapa mimba wanafunzi na wanaokubali
kuwaozesha.
"Rais Magufuli alishatoa agizo kuwa sasa
hivi wanafunzi wasome bure, hivyo badala ya kutumia fursa hiyo wazazi na walezi
wanawaozesha wasichana au kuwachungisha mifugo wavulana, hao wote
nitawachukulia hatua kali," alisema Mofuga.
Mmoja kati ya wakazi wa mji wa Mbulu, Yohana
Amnaay alisema jamii inapaswa kuunga mkono zaidi juhudi zilizoonyeshwa na mkuu
huyo wa wilaya ili wanafunzi wa kike wapate elimu bora.
"Suala la kwenda kwa mazoea hivi sasa
limekwishwa kwani tumeona juhudi za mkuu wa wilaya kupiga vita watoto wa kike
kupata mimba na kuwachukulia hatua wanaowapa mimba wanafunzi," alisema
Amnaay.
NAIBU WAZIRI WA MALISILI NA UTALII,MHANDISI RAMO MAKANI AZUNGUMZA NA WAKAZI WA KIJIJI CHA MSHIRI WILAYANI MOSHI KUHUSU ENEO LA NUSU MAILI
WEDNESDAY, AUGUST 2, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba akiongozana na Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani walipotembelea kijiji cha Mshiri katika wilaya ya Moshi kusikiliza Changamoto zinazo wakabili wananchi waishio kando ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro .
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwa na Mbunge wa Jimbo la Vunjo,James Mbatia katika mkutano wa wananchi katka kijiji cha Mshiri wilayani Moshi uliohusu Zaidi changamoto iliyopo katika eneo la Nusu Maili katka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro .
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mshiri wilayani Moshi waishio kando ya Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro waliofika kwa ajili ya kumueleza Naibu Waziri wa Malisli na Utalii,Mhandisi Ramo Makani changamoto zinazowakabili hususani eneo la Nusu Maili.
Niabu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mshiri wilayani Moshi ,alipotembelea kijiji hicho kusikiliza Changamoto zinazo wakabili hususani katika eneo la Nusu Maili lililopo chini ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Mshiri wilayani Moshi wakimsikiiza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani (Haupo pichani ) alipozungumza nao.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ilipo kijiji cha Mshiri ,James Mbatia akizungumza katika mkutano huo kuhusu Changaoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kaika kijiji hicho.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mshiri wilani Moshi.
Mku wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba akizungumza katika mkutano huo.
Baadhi ya viongozi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) walioongozana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani kutembelea kijiji cha Mshiri,kutoka kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete,Meneja Utalii wa Tanapa.Bw Manase na Mhifadhi Ujirani Mwema KINAPA,Bi Hobokela Mwamjengwa.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifdhi za Taifa (TANAPA) Mtango Mtahiko akiwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook katika mkutano wa Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani na wananchi katika kijiji cha Mshiri.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA,Mtango Mtahiko akitoa salamu katika mkutano huo.
Baadhi ya Wananchi katika kijiji cha Mshiri.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook akizungumza jambo katika mkutano huo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini
RC RUKWA ZELOTE STEPHEN AZIONYA HALMASHAURI
RC Rukwa Mh. Zelote Stephen akiwaonesha waheshimiwa madiwani (hawapo pichani)risiti ambazo tayari zimeshakatwa kabla ya kutumiwa.
RC Rukwa akiwaonesha waheshimiwa madiwani (hawapo pichani) kitabu cha hoja za mthibiti na mkaguzi wa serikali kwa Manispaa ya Sumbawanga.
RC Rukwa akitoa ufafanuzi.
…………………………….
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amezionya halmashauri zote mkoani Rukwa kuhakikisha wanazitumia vizuri manshine za EFD kwa kuongeza mapato katika halmashauri zao.
Ametoa onyo hilo kwenye kikao maalum cha kujibu hoja za ukaguzi wa hesabu za serikali kwa madiwani wa Manispaa ya Sumbawanga katika kumalizia ziara yake maalum kwa halmashauri zote mkoani humo kujua namna Halmashauri zilivyojipanga ili hoja hizo zisijirudie miaka inayofuata.
Akiongea huku akionesha risiti alizozikamata katika maeneo mbalimbali ya mauzo alisema kuwa serikali inafanya kila liwezalo katika kuhakikisha inakusanya maopato lakini bado kuna watumishi wanatafuta namna ya kuiskosesha serikali mapato hayo.
“katika kila sehemu za mauzo lazima mashine hizi ziwepo na kuwepo sio mtindo huu (akionesha msururu wa risiti zilizokatwa tayari kwa matumizi) hizi nimezikamata maeneo anajua Mkurugenzi, asubuhi watu wanagawana, ndio mchezo uliopo, pamoja na jitihada tunazofanya bado watu wanatafuta mbinu za kuiba, hii sio kwamba nimeleta iwe mfano, hapana, nimezikamata na mfahamu kuwa mimi ni mtaalamu wa kukamata,”Alisema
Katika Kusisitiza suala la uwazi wa matumizi ya fedha za halmashauri kwa waheshimiwa madiwani Mh. Zelote alitaja majukumu kadhaa ya Mkurugenzi wa Halmashauri na kusema kuwa moja ya kazi za Mkurugenzi ni kuhakikisha kuwa madiwani wanapata taarifa za fedha za halmashauri.
“Hapa mmezungumza na mmenionyesha kwa kiasi kikubwa kwamba hamnazo taarifa na nikiangalia kazi moja wapo ya waheshimkwa madiwani ni kiusimamia matumizi ya fedha za halmashauri zao sasa mtasimamiaje ikiwa hamna taarifa,” Alisema.
Na kukumbusha kuwa Mkurugenzi ndio katibu wa kamati ya fedha ya halmashauri lakini na kuonya kuwa kamati hiyo ibebe sura ya halmashauri na sio sura ya kamati na kuwasisitiza kufuata taratibu nyingine za ikiwa kurudisha mrejesho kwa wengine juu ya mipango na maazimio yaliyofikiwa.
Katika kikao hicho Mh. Zelote alimtambulisha mtaalamu wa TEHAMA ili awaelezee waheshimiwa madiwani namna mifumo ya fedha inavyofanya kazi ili nao wawe na uelewa mpana katika kufuatilia mapato na matumizi ya halmashauri.
“Suala la kukusanya mapato limekuwa likiimbwa asubuhi, mchana na usiku, kuwa tuhakikishe tunajipanga vyema kukusanya mapato ya halmashauri kwa kupitia utaratibu uliopo, suala la kutumia hizi mashine sio la kuhoji tena mwisho ulikuwa mwezi wa tatu ndio agizo lililopo kwa wakurugenzi kuwa mashine hizi ziwepo na zinafanya kazi,” Alisema.
Na katika kuhakikisha kuwa vitabu hivyo havipati nafasi Mh. Zelote alitoa siku saba vitabu hivyo kurudishwa maghalani na kuongeza kuwa watumishi wanaokiuka miiko ya kazi zao kuwajibishwa kulingana na madhara waliyosababisha na kuwaasa kujenga uaminifu katika utumishi ndani ya halmashauri.
“Sitaki kusikia tena kuwa kwenye mkoa wangu kuna halmashauri inanyooshewa kidole, mmeshanyooshewa kidole mara moja sitaki kuona tena hicho kidole,” alimalizia.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya nSumbawanga Mh. Julieth Binyura alishanngazwa na wataalamu hao kushindwa kudhiti hoja na hatimae wao kuwa chanzo kikuu cha kuzalisha hoja.
“Mtu kama unaitwa mtaalamu na serikali imekuamini kwanini tena unaizalishia serikali hoja, na suala la fedha ni suala nyeti sana hivyo linahitaji umakini wa haloi ya juu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma inayostahili na si vinguinevyo,” Alisema.
Akifunga kikao hicho Mstahiki meya wa Manispaa ya Sumbwanga Mh. Justin Malisawa alimuahidi Mkuu wa Mkoa kusimamia yale yote aliyoyaelekeza na kuomba msaada wake pindi pale watakapokwama.
Subscribe to:
Posts (Atom)

























































