Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Starnley Kamoga akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Haydom juuu ya kuchangia maendeleo yao.
Saturday, 20 May 2017
DC MBULU AWAASA WANANCHI
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara,
Chelestino Mofuga amewataka wakazi wa Kijiji cha Guye kuacha malumbano na
kujenga madarasa ya shule ya msingi kwa muda wa mwezi mmoja.
Mofuga akizungumza na wananchi wa kijiji
hicho, alisema anahitaji apatiwe mpango wa maendeleo wa kijiji, apatiwe taarifa
hiyo ofisini kwake ikiwemo kujenga madarasa kwa mwezi mmoja.
Alisema pamoja na serikali kuwa na sera ya
elimu bure na elimu bila malipo lakini wananchi wanapaswa kujenga madarasa ya
shule ili wanafunzi wao waweze kupata elimu kwenye mazingira mazuri.
“Ni kijiji cha ajabu kweli kweli, yaani ninyi
mnakaa mwaka mzima lakini hakuna shughuli za maendeleo, kule watoto wanasoma
wenu wanasoma kwa mazingira magumu ya madarasa,” alisema Mofuga.
Alisema endapo kuna mapungufu mengine kwenye
shule hiyo ikiwemo nyumba za walimu, wananchi hao wanapaswa kuhakikisha
yanajengwa kwani hiyo ni kwa jaili ya faida ya watoto wao.
Mkazi wa kijiji hicho cha Guye, John Akonaay
alisema anasikitishwa na kitendo cha baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kuwa na
mwamko mdogo wa kuchangia kutokana na ufujaji wa fedha uliofanyika.
“Tunashukuru mkuu wa wilaya leo (juzi)
umeagiza yule mtendaji wa kijiji aliyefuja fedha zetu amekuja na kujibu tuhuma
kuwa atazilipa ila tukichanga tena huyu mtendaji mpya asizifuje,” alisema
Akonaay.
Mkazi mwingine wa kijiji hicho Adam Sule
alisema anasikitishwa na kitendo cha kuambiwa kuwa wakili aliyekuwa anafuatilia
kesi ya ufujaji wa fedha za kijiji anawadai sh1.5 milioni hivyo walipe.
“Tulishamlipa huyo mwanasheria lakini hivi
sasa bado tunaambiwa tunadaiwa ili hali kwenye taarifa ya awali inaonyesha
alishalipwa sh150,000 ya usafiri wa kutoka Babati hadi hapa,” alisema Sule.
MWISHO.
Friday, 7 April 2017
WATAKIWA KUWAUNGA MKONO WAWEKEZAJI
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Sipitieck amewataka wakazi wa Mji mdogo wa
Mirerani kuwapa ushirikiano wawekezaji wa TanzaniteOne na siyo kuwabeza.
Sipitieck amesema wananchi wa mji mdogo wa
Mirerani wanapaswa kuwa wazalendo kwa kuwaunga mkono na kushirikiana na
wawekezaji wa kampuni ya TanzaniteOne kuliko kuwavunja moyo.
Aliyasema hayo juzi wakati akiushukuru uongozi
wa kampuni ya TanzaniteOne waliotoa ahadi ya msaada wa kujenga madarasa saba ya
shule ya msingi Songambele ambayo madarasa yake yaliharibika.
Alisema baadhi ya wananchi wa eneo hilo
wamekuwa na kigeugeu kwani wakati mwingine kuwabeza wawekezaji hao na siku
inayofuata huisifu TanzaniteOne, hivyo wawe na msimamo mmoja unaoeleweka.
“Nadhani ifike mwisho kwa wananchi kuwabeza
wawekezaji ambao hutumia nafasi yao kwa kusaidia jamii katika baadhi ya miradi,
kupitia kile wanachokipata kwenye uwekezaji huo,” alisema Sipitieck.
Alisema awali halmashauri hiyo ilitaka
kuhamisha shule hiyo ambayo tangu mwaka 2013 iliharibika baada ya kupitiwa na
mafuriko makubwa ila kampuni hiyo imeahidi kuijenga upya kwa ubora zaidi.
Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Faisal
Shabhai alisema ana imani kubwa kuwa wataendelea kushirikiana jamii ya eneo
hilo na kampuni hiyo katika kuhakikisha wanawezesha miradi ya jamii.
“Hivi sasa tunafungua ukurasa mpya kwa
kushirikiana nanyi kama kawaida kwa kuhakikisha kile kidogo tunachokipata
tunakigawa kwa jamii inayozunguka sehemu ya uwekezaji wetu,” alisema Shabhai.
Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani
Adamu Kobelo alisema wananchi wa eneo hilo wanapaswa kuweka kipaumbele kwenye
miradi ya jamii na siyo mtu mmoja mmoja kupewa fedha.
Mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo, Japhary
Matimbwa alisema anaishukuru kampuni ya TanzaniteOne kwa kusaidia baadhi ya
miradi ikiwemo kuichimbia kisima shule ya awali na msingi Kazamoyo.
“Wapo watu ambao kipindi cha uwekezaji wa
mzungu walikuwa wanapiga bomu na kujinufaisha wenyewe ila sasa hivi wamekuja
wawekezaji wazuri ila wachache wanapinga,” alisema Matimbwa.
Wednesday, 5 April 2017
MJASIRIAMALI EMBOREET
Mjasiriamali wa Kijiji cha Emboreet Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara, Estar Lemwanda akizungumza juu ya changamoto ya
ujasiriamali kwenye eneo hilo ili kujiinua kiuchumi.
Subscribe to:
Posts (Atom)

