Sunday, 14 December 2014

WANAMSIMIKA KIONGOZI WAO



Wananchi na wazee wa kimila wa Kijiji cha Kambi ya Chokaa, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakimsimika Joshua Kuney kuwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho, baada ya jina lake kukatwa na viongozi wa CCM wa Wilaya hiyo na kumshinda Mbuki Mollel kwa kura 335 kwa 215.



Wakazi wa Kijiji cha Kambi ya Chokaa, Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiandamana kwenda ofisi ya Serikali ya Kijiji kumsimika Joshua Kuney kuwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho, ambaye awali katika kura ya maoni ya CCM alishinda na jina lake kuenguliwa, alipata kura 335 na kumshinda Mbuki Mollel aliyepata 215.

Wananchi wa Kijiji cha Kambi ya Chokaa, Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiandamana kwenda ofisi ya Serikali ya Kijiji kumsimika Joshua Kuney kuwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho, ambaye awali katika kura ya maoni ya CCM alishinda na jina lake kuenguliwa, alipata kura 335 na kumshinda Mbuki Mollel aliyepata 215

Saturday, 13 December 2014

KAMPENI CCM



Kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Kata ya Mirerani.

Friday, 12 December 2014

KAMPENI CCM


Wagombea 12 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Vitongoji vya kata ya Endiamtu, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, waliopita bila kupingwa wakiwasikiliza wagombea nane wa vitongoji vya kata ya Mirerani.
Baadhi ya wagombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM wa kata ya Mirerani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye mkutano wa kampeni kwenye kata hiyo.

Saturday, 6 December 2014

MKUTANO WA CHADEMA


Mgombea Uenyekiti wa Kitongoji cha Tunduru, Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Chengula akinadi sera za Chadema kwenye mkutano wa kampeni.

Wakazi wa Kitongoji cha Tunduru, Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakimsikiliza mgombea Uenyekiti Christopher Chengula akinadi sera za chama hicho kwenye mkutano wa kampeni.

Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Ambrose Ndege akizungumza na wakazi wa Kitongoji cha Tunduru, wakati akinadi sera za chama hicho kwenye mkutano wa kampeni.

Mgombea Uenyekiti wa Kitongoji cha Kazamoyo Juu David Kyara, akizungumza na wakazi wa Kitongoji cha Tunduru, Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema.