Saturday, 6 December 2014

MKUTANO WA CHADEMA


Mgombea Uenyekiti wa Kitongoji cha Tunduru, Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Chengula akinadi sera za Chadema kwenye mkutano wa kampeni.

Wakazi wa Kitongoji cha Tunduru, Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakimsikiliza mgombea Uenyekiti Christopher Chengula akinadi sera za chama hicho kwenye mkutano wa kampeni.

Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Ambrose Ndege akizungumza na wakazi wa Kitongoji cha Tunduru, wakati akinadi sera za chama hicho kwenye mkutano wa kampeni.

Mgombea Uenyekiti wa Kitongoji cha Kazamoyo Juu David Kyara, akizungumza na wakazi wa Kitongoji cha Tunduru, Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema.

Saturday, 29 November 2014

NAWAKABIDHI SARUJI



Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo ( wapili kulia) akiwakabidhi Diwani wa Kata ya Ganana, Wilayani Hanang’ Zacharia Tarmo na Diwani wa viti maalum Juliana Songai, moja kati ya mifuko 100 ya saruji yenye thamani ya sh1.7 milioni iliyotolewa na wakuu wa idara wa halmashauri ya wilaya hiyo, kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo Christina Mndeme na katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Filex Paul Mabula.

TUNAFUATILIA BUNGE



Wananchi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakifuatilia kikao cha Bunge.

Tuesday, 25 November 2014

MAPUNDA APOKEWA MBINGA

Msafara wa vijana wakereketwa wa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wakimpokea Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Sixtus Mapunda.
 

WANAFUNZI

Mmoja kati ya wanafunzi wa vyuo vilivyopo hapa nchini, ambaye hutumia miili yao kwa ajili ya umalaya.