Sunday, 7 July 2013

WATANO WAFA KWENYE MACHIMBO YA TANZANITE

                                                                                

Wachimbaji wadogo watano wa madini  ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani,Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha mchanga wakiwa mgodini. 

Katika tukio la ajali hiyo iliyotokea Julai 6 mwaka huu saa 1 jioni,kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite Mirerani ,wachimbaji hao watano walifariki dunia papo hapo na mchimbaji mmoja akajeruhiwa kwenye tumbo na mbavuni.



Akithibitisha kutokea tukio hilo,Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi,Akili Mpwapwa aliwataja waliofariki dunia ni Goodlove Zablon (35) na Ndekirwa Kitoi (33) wakazi wa Makiba Wilayani Arumeru.

Kamanda Mpwapwa aliwataja wachimbaji wengine waliofariki ni Jackson  Kavishe (45) mkazi wa Mirerani,Emmanuel John (33) mkazi wa Makiba na Emmanuel Joshua (40) mkazi wa Nkwoaranga wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Alisema mchimbaji mwingine Sifael Simba (30) mkazi wa kijiji cha Maroroni wilayani Arumeru alijeruhiwa kwenye mbavu na tumboni ambapo amelazwa kwenye hospitali ya mkoa wa Arusha,Mount Meru.

Tuesday, 2 July 2013

OBAMA AMALIZA ZIARA YAKE TANZANIA



 Rais Barack Obama wa Marekani akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete,wakati akijiandaa kuondoka kwenye ardhi ya Tanzania baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini na kurudi Marekani.  



Rais Barack Obama wa Marekani na Rais Jakaya Kikwete wakishangiliwa na baadhi  ya watanzania waliofika kumpokea Rais Obama alipokanyaga ardhi ya Tanzania.

Monday, 1 July 2013

NEIMAR

                                                                               

Mchezaji wa timu ya Taifa ya Brazil,Neimar akibusu kombe la mabara baada ya kuifunga timu ya Hispania

NYALANDU NA OHAYODA

                                                                                   

             Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu  akikamata gazeti la Ohayoda linalotengenezwa mji mdogo wa Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara (katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ohayoda,Amani Paulo na Mchungaji kiongozi wa KKKT Usharika wa Haydom,John Nade