AMUUA MKEWE KWA WIVU WA MAPENZI
Ikiwa leo ni siku ya wapendanao mkazi wa Kijiji cha Dirimu Wilayani Mbulu Mkoani
Manyara, amemuua mkewe kwa kumchinga shingo kama kuku na yeye kujiua kwa
kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Mwanaume
huyo ambaye amezaa watoto nane na mke wake, inadaiwa kuwa walikuwa wanaishi
nyumba moja ila baba alikuwa akitoka nyumbani asubuhi anarudi usiku na hajui
familia yake imeshindaje wala imekula au haijala chakula.
Akizungumza na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara,
SSP Christopher Fuime alisema vifo hivyo vilitokea Februari 12 saa 10 jioni
kwenye pori la kijiji cha Dirimu katika wilaya ya Mbulu.
Kamanda
Fuime aliwataja marehemu hao kuwa ni Qambadu Kwatlema (45) mkulima na mkazi wa
kijiji hicho ambaye alimuua mke wake Amsi Matle (43) kwa kumchinja na kisu
shingoni na kumkatakata sehemu nyingine za mwili.
“Chanzo
cha vifo ni wivu wa kimapenzi kwani mwanaume alihisi mke anatoka nje ya ndoa
yao na inasemekana siku moja kabla ya kifo chake Kwatlema alisema atamuua
hawara yake au kumuua mkewe,” alisema Kamanda Fuime.
Alisema
baada ya Kwatlema kumuua mkewe naye alikimbilia porini jirani kidogo na
wanapoishi na kujinyonga na miili ya marehemu hao imeshazikwa kwenye eneo moja baada
ya uchunguzi wa miili hiyo kufanywa na daktari na polisi.
Hata
hivyo, mmoja kati ya shuhuda wa tukio hilo Daudi Yuda alidai kuwa jana yake
kabla ya tukio hilo, Kwatlema alikuwa anamlalamikia jirani yake ana mahusiana
na mkewe hivyo atafanya jambo ambalo litaacha historia kwao.
“Sisi
tulidhani ni utani anaongea wakati akinywa pombe na kulewa kumbe mwenzetu
alikuwa na wivu kweli ila hakuweza kumuua mtu aliyekuwa anahisi anatembea na
mke wake akaishia kumuua mkewe,” alisema Yuda.
Naye,
Scolastika Sulle alisema wakazi wa eneo hilo wamesikitishwa na vifo hivyo vya
kikatili, kwani Kwatlema alimuua kwa kumchinga kama kuku na kumtoa utumbo nje
baada ya kumkata na kumuachia shimo mgongoni.
“Watoto
nane wameachwa yatima bila wazazi lakini pia mtoto mdogo wa mwisho mwenye umri
wa miaka mitatu ndiye anayewasikitisha wananchi wa kijiji hiki kwani wameachiwa
majonzi makubwa sana,” alisema Sulle.